Na Shani Ramadhani KUFUATIA
varangati lililotokea Tabora katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014,
baada mpenzi wa mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’,
Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kukataliwa na mashabiki, Shilole ameamua
kufunguka kuwa Nuh atabaki kuwa mpenzi wake katika hali yoyote.
Akizungumza na paparazi wetu, Shilole
alisema lengo lake lilikuwa ni kumtambulisha mpenzi wake kwa mashabiki
wake japo walimkataa kuwa shemeji yao.
“Wakati namtambulisha Nuh kwa wakazi wa Tabora kuwa shemeji yao kiukweli nilishindwa kuelewa kwa nini nilizomewa ila ninachoweza kusema tena wakubali, wakatae Nuh atabaki kuwa shemeji yao tu,” alisema Shilole.
CHANZO: GPL

No comments:
Post a Comment