Mchepuko? Baada ya kuachana na mkewe, Halima Ally, staa wa Nyota ya Chipsi Mayai na Prodyuza wa Sharobaro Records, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ amenaswa live na mrembo anayejulikana kwa jina la Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ ambaye ni msanii wa filamu, wakiwa katika mahaba nipoteze kama ndege ya Malaysia.
Staa
 wa Nyota ya Chipsi Mayai , ‘Bob Junior’ akiangusha busu shavuni mwa 
mrembo anayejulikana kwa jina la Sabrina Omary ‘Sabby Angel’
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Sabby 
ambaye ndiye aliyevujisha picha za tukio hilo, Sabby na Bob Junior kwa 
sasa wako katika mahaba mazito na ni watu wanaopendana kwa sababu kila 
unapomuona Sabby yupo karibu na mwanamuziki huyo.
“Sasa hivi Sabby na Raheem ndiyo habari ya 
mjini kwani kila sehemu wapo pamoja na wanapendana sana,” alidai rafiki 
huyo wa Sabby.Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba wawili hao 
wanaweza kuvalishana pete ya uchumba muda wowote kuanzia sasa.
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Bob 
Junior ambaye hakupatikana lakini alipotafutwa Sabby ili kusikia kauli 
yake kuhusu uhusiano wake na Bob Junior alikiri na kusema kuwa ni mtu 
ambaye anampenda na ndiye anamfanya awe na furaha.
CHANZO: GPL 


No comments:
Post a Comment