EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, October 1, 2014

Mkasi TV yamuhoji Gardner G. Habash… Aliyoyaongea ni Pamoja na Haya.

Mtangazaji Gardner G. Habash ni miongoni mwa Watangazaji hodari ambao Tanzania imewahi kuwa nao ambapo alianza kwa kusikika kupitia CloudsFM kwenye shows mbalimbali ikiwemo Jahazi kabla ya kuanza kazi.
Wakati huu ambapo kumekua na stori zilizoenea mtaani kuhusu yeye na ndoa yake pia kazi, show ya TV ya Mkasi inayoongozwa na mtangazaji Salama Jabir imepata nafasi Exclusive ya kuongea nae.
Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya sentensi alizoziongea Captain G kwenye Mkasi on EATV.

Kwanza alianza kwa kuongelea jinsi alivyoingia kufanya kazi Redioni huku akimkumbuka Othman Njaidi aliemchukua na kumpeleka CloudsFM sio kama mtangazaji bali akajiunge na timu ya Marketing, akakutanishwa na Ruge Mutahaba aliekua General Manager wakati huo ambae alipoisikia tu lafudhi ya Gardner akasema huyu anafaa kuwa mtangazaji.

Staa aliefurahi baada ya kukutana nae ni D’Banj wa Nigeria, alifurahia uchangamfu wake…
Salama alipomuuliza kuhusu uhodari wake wa kutangaza habari za mastaa wa dunia… Captain G. akasema ‘nilikua nanunua majarida kwenye maduka yanayouza majarida kutoka nje, wakati Internet hamna kulikua na majarida mengi kidogo’

‘Mimi ni mchaga kabisa wa Baba na Mama lakini Wazazi wangu walihamia Tanga zamani alafu mimi nimezaliwa Ngamiani pale Hospitali na tukaishi Chumbageni muda mrefu kwa hiyo nilipata lafudhi ya Tanga pale, na hiyohiyo lafudhi ya Tanga ndio iliyonipa kazi kwenye Radio’

Salama akamuuliza ‘Unajisikiaje ukisikia mtu anatangaza kama wewe‘ >> Gardner akajibu ‘kuna baadhi ya watu kusema ukweli wanachukizwa sana na hicho kitu na wananilalamikia sana kwamba kuna Watangazaji wengi wamekua wanakuiga kwenye kutangaza Redioni na kwenye kutengeneza jingle kama za kwako lakini mimi nimeiona ni baraka kwangu, kama watu wamekupenda kiasi kwamba wanakuiga ni jambo la kufurahisha kwangu mimi linanifurahisha sana’

Kuhusu kitu kilichomfanya akaondoka kwenye Radio, Captain amesema ‘Nilifanya kazi miaka 9 akili ikawa imechoka nikafikiria lazima pia nifanye biashara watu wanakusifia kwamba una uhodari flani kwa hiyo unajipa challenge kwanini nisitengeneze kitu changu, ndio tukafungua biashara za chakula lakini zaidi nilikua nataka kupumzika’

Swali jingine kutoka kwa Salama likawa ‘nasikia kuna stori kwamba hivi karibuni pia unaweza kurudi kule ama ukaenda sehemu nyingine‘ Captain G. akajibu >>> ‘ni mmoja kati ya hao wawili, stori ni ya ukweli ndio maana naondoka, nimemaliza mkataba nimepata ofa nyingine kubwa naichukua’

Swali jingine lililokua linasubiriwa ni hili alilouliza Salama >> ‘kuna stori mtaani kwamba wewe na Lady Jaydee mmeachana’  Gardner akajibu ‘mimi sijawahi kupata interview muda mrefu sana… nadhani hii inaweza kuwa interview yangu ya kwanza, kwahiyo nilikua nataka nikuombe tuongee kuhusu mimi kwanza manake tukizungumzia kuhusu JayDee nitafunikwa hapa’

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate