EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, November 12, 2014

DIAMOND, ZARI MAHABA MAZITO

 
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
Siku chache baada ya kumwagwa na Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’, Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amenaswa kwenye mahaba mazito na msanii, mtangazaji, mjasiriamali, tajiri na mrembo mkali kuliko wote Afrika Mashariki,  Zarinah Hassan a.k.a Zari au Boss Lady.
Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akimhagi msanii mrembo mkali kuliko wote Afrika Mashariki,  Zarinah Hassan a.k.a Zari au Boss Lady.
HABARI YA TAUNI
Habari ya ‘mujini’ ilidai kwamba, mahaba ya wawili hao yalianzia safarini walipokutana kwenye ndege moja wiki iliyopita ambapo Diamond alikuwa akitokea nchini Nigeria kupitia Afrika Kusini kisha Dar huku Zari akitokea Afrika Kusini kuelekea Dar kibiashara.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mastaa hao walipokutana kwenye ndege waliungana na kupiga picha za pamoja kisha safari yao ya mahaba niue ikaanzia hapo.
UWANJA WA NDEGE    
Chanzo hicho kilimwaga ‘ubuyu’ kwamba, wawili hao walipotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Diamond alionekana akiwa ‘veri klozi’ na Zari kiasi cha kuibua minong’oni uwanjani hapo kwa namna walivyoonekana wamependezeana.
Diamond Platnumz akipozi na mrembo Zari kimahaba.
KWENYE GARI LA DIAMOND
Ilisemekana walipofika nje walikwenda moja kwa moja kwenye maegesho ya magari (parking) kisha walizama kwenye ndinga la staa huyo wa Ngoma ya Mdogomdogo ambapo waliongozana hadi hotelini.

WENYEJI WA ZARI
“Boss Lady alifuatwa na wenyeji wake lakini cha kushangaza walishindwa kumpokea kwani baada ya kumuona yuko kwenye mahaba na Diamond nao wakajikata kiaina,” alisema sosi wetu.
HOTELINI UFUKWE WA BAHARI YA HINDI
Mtoa ubuyu wetu huyo aliendelea kunyetisha kwamba, baada ya kutimka airport, siku ya kwanza walilala hoteli moja maarufu jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sababu maalum) iliyopo kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi.
‘Diamond Platnumz’ akiwa na mrembop huyo kwenye 'pipa'.
WASHTUKIWA, WAHAMA HOTELI
Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa Diamond au Dangote, kilizidi kuvujisha kwamba, ilipofika usiku, wawili hao waliamua kuhama kwenye hoteli hiyo kwa madai kwamba walikuwa wameshtukiwa na watu wengi hivyo walihofia kunaswa.Ilisemekana kwamba walihamia hoteli nyingine ambayo nayo ipo pembezoni mwa ufukwe huo.
KOSA LA KIUFUNDI
Katika harakati zao zote, kosa la kiufundi walilofanya ni kujifotoa wakiwa kimahaba ufukweni na kuziachia picha hizo kwenye mitandao ya kijamii huku wakisifiana.
MASHABIKI
Mashabiki wa jamaa huyo kupitia mitandao hiyo, walidai kwamba huenda Diamond mwenye umri wa miaka 26, amefanya hivyo ili kumkomoa Wema ambaye alimtosa Dangote kistaarabu.
Walidai kwamba Zari anaweza kumtangaza zaidi Diamond kimataifa na hasa Uganda tofauti na Wema ambaye angemtangaza Bongo tu.
Mrembo Zari au Boss Lady akiteta jambo.
NENO
“Diamond mjanja sana. Kenya alizua gumzo na msanii Avri na yule demu wa Malindi, Mombasa na baadaye msanii Victoria Kimani.
NIGERIA
“Kule Nigeria alishakuwa gumzo na akina Davido, Iyanya, Tiwa Savege na Yemi Alade ambaye walikutana Coke Studio Africa jijini Nairobi, Kenya.
NI ZAMU YA UGANDA
“Ishu ilikuwa Uganda lakini sasa ni kama ananawa maana ameshapata ‘kiki’ kupitia Zari,” alisema mmoja wa wachambuzi wa habari za mastaa Bongo.
DIAMOND ANASEMAJE?
Baada ya kunyetishiwa mchongo huo, waandishi wetu walimvutia waya Diamond asubuhi, mchana, jioni na usiku lakini simu haikupokelewa.Zari ni mzawa wa nchini Uganda ingawa ana uraia wa Afrika Kusini ambapo anaishi kwa sasa.
Mkali Zari akiwa na ndinga yake aina ya Black Chrysler (2008).
UTAJIRI WA ZARI
Pamoja na uzuri wa umbo na sura ikiaminika kuwa ndiye msanii mrembo mkali Afrika Mashariki, Zari ndiye msanii tajiri wa kike namba moja nchini Uganda kwa kuwa ana utajiri wa kutisha.
Zari ana umri wa miaka 32 (anamzidi Diamond kwa miaka 6), akiwa ni mama wa watoto wawili, aliyeolewa na Ivan Semwanga ambaye mwaka jana ndoa yake ilidaiwa kuingia mdudu japo haijavunjika, hivyo bado ni mke wa mtu.
Zari anaingiza mshiko mrefu akimiliki majumba yanayomwingizia fedha ndefu na magari ya kifahari kama yale ya mastaa wa Kimarekani.
Zari amepata mafanikio makubwa  katika muziki na kipindi chake cha The Boss Lady kwenye Runinga ya UBC nchini humo, kinachomuingizia mkwanja mrefu kutokana na matangazo kikifananishwa na kile cha mwanamitindo wa Marekani, Kim Kardashian cha Keep Up With The Kardashians.
 Kwa mujibu wa Jarida la Times la Uganda, huenda Zari akaingia kwenye orodha ya wanawake matajiri zaidi Afrika siku chache zijazo endapo ataendelea kuzichanga.
Aliyekuwa baby wa ‘Diamond Platnumz’, Wema Sepetu akipozi.
MAGARI
Zari mwenye maskani yake Kampala na Afrika Kusini, anamiliki ndinga kibao za kisasa na zenye thamani kubwa kama BMW (2006) lenye thamani ya dola 47,000 (Sh. milioni 75.2), Black Chrysler (2008) linalouzwa dola 16,000 (Sh. milioni 25.6) na Audi Q7 (2010) linalogharimu dola 53,000 (Sh. milioni 84.8).
Mengine ni Silver Chrysler (2008) lenye thamani ya dola 13,000 (Sh. milioni 20.8), Jetta Volkswagen (2006) linalogharimu dola 27,000 (Sh. milioni 43.2), Mercedes Benz Convertible (2008) linalouzwa dola 26,000 (Sh. milioni 41.6), Range Rover Sport (2010) lenye thamani ya dola 109,000 (Sh. milioni 174.4), Lamborghini Gallardo (2010) linalogharimu dola 198,000 (Sh. milioni 316.8), Hummer H2 la dola 150,000 (Sh. milioni 240) na mengine mengi, yote yakiwa na jina lake badala ya namba za usajili.
Pia Zari anamiliki maduka, hoteli na majumba ya kisasa kwenye miji mikubwa ya Pretoria na Cape Town nchini Afrika Kusini na Kampala, Uganda. Kazi ni kwako Diamond!

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate