Aliyekuwa rais wa mpito nchi ya Zambia, Guys Scott.
Chama tawala nchini Zambia (PF) kimemtimua kaimu rais wa nchi hiyo Guys Scott kutoka chamani na kuvunja utaratibu wa katiba.
Taarifa
hii ni kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho. ''Amekuwa akiwaajiri na
kuwafuta watu kazi ovyo na pia bila ya kushauriana na kamati kuu ya
chama,'' amesema Malozo Sichone.
Bwana Scott, ambaye licha ya hatua hiyo ataendelea kuwa mwanachama wa
chama hicho, ataendelea kuhudumu kama kaimu rais hadi uchaguzi
utakapofanyika tarehe 20 Januari.Scott aliteuliwa kuwa kaimu rais
kufuatia kifo cha hayati Rais Michael Sata aliyefariki mwezi jana.
(CREDIT: BBC SWAHILI)
No comments:
Post a Comment