EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, November 15, 2014

MGAWO MALI ZA JIDE, GARDNER UTATA

Stori: Mwandishi Wetu HALI tete! Bado vuguvugu la madai ya kuvunjika kwa ndoa ya mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteni’ na Mbongo Fleva, Judith Daines Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee au Jide’, sasa lingine limeibuka ambapo mali za wawili hao zinatajwa kuzua utata, Risasi Jumamosi  linachambua.
Mbongo Fleva, Judith Daines Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee au Jide.
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani, Gardner ameshapeleka hati ya kesi kwa mwanasheria wake kwa kusudio la kumpandisha kizimbani mtalaka wake huyo ili mgawo wa mali ujulikane na kila mmoja apate haki yake.

KILICHOZINGATIWA
Kilichozingatiwa katika mgawo huo ni uhalali wa ndoa yao iliyofungwa Mei 14, 2005 ambapo mali zote zilizopatikana ndani ya ndoa ni za wote kwa mujibu wa sheria ya Ndoa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nyumba anayomiliki Judith Daines Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee na aliyekuwa mumewe Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteni.
“Gardner anataka mgawo wake, lakini sasa utata ulioibuka ni kwamba, inaonekana kama mali zote ni za Jide kwa vile zimeandikwa majina yake hivyo jamaa ana wasiwasi kwamba Jide anaweza kusema mahakamani kuwa alizichuma mali hizo kabla ya ndoa,” kilisema chanzo hicho kilicho jirani na familia hiyo.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, utata huo umemfanya Gardner kuwa bize ili kuhakikisha anaumaliza hususan kwenye nyumba yao iliyopo Mbezi ambapo wengi wanaamini ilijengwa kwa kutumia fedha ya Jide kabla hawajafunga ndoa.
MALI ZINAZOTAJWA
Mali zinazotajwa kuibua utata ni Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Kinondoni, Dar ambao hivi karibuni Jide aliubadili jina na kuuita M.O.G Restaurant. Mgahawa huo walipangishwa na mtu.
Gari aina ya Range Rover Evoque linalomilikiwa na Judith Wambura ‘Lady Jaydee.
Kuna madai kwamba, Jide na Gardner kabla ya ndoa yao kuparaganyika walikwenda kwa mmiliki huyo na kusema wameamua kuuacha baada ya mkataba wao kumalizika. Lakini kilichoonekana baadaye, Jide alirudi kwa njia ya uani na kuanzisha mkataba mpya bila Gardner na kuuita M.O.G.
Mali nyingine mbali na nyumba na mgahawa ni mabasi madogo mawili aina ya Toyota Hiace, moja la Machozi Band na la M.O.G Restaurant. Mabasi hayo yameandikwa Lady Jaydee & Machozi Band. Hata hivyo, yapo madai kwamba Machozi Band nayo imebadilishwa jina, sasa inaitwa Lady Jaydee & The Band.
Mali nyingine ni Albamu zote za Jide alizotoa tangu mwaka 2005 wakiwa tayari kwenye ndoa ambapo kwa kawaida mauzo yake ni endelevu na gari la kutembelea aina ya Range Rover Vogue.
Albamu hizo ni  Moto (2005),  Shukrani, The Best of Lady Jaydee (2006) na Nothing But the Truth (2014).
la M.O.G Restaurant inayomilikiwa na Judith Wambura ‘Lady Jaydee.
KAMA NI KUPATA
Chanzo kinabainisha kuwa, uhakika wa mali anazoweza kupata Gardner ni mgawo wa pesa kwa mauzo ya gari hilo la kutembelea na nyumba ambapo inaaminika ndiyo mali ya kifamilia zaidi. 
SHERIA YA TALAKA
Risasi Jumamosi lilitembea ofisi za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Rita) jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujua sheria za talaka zinasemaje!
1. Mwenza mwenye nia ya kuomba ndoa ivunjwe anatakiwa kupeleka malalamiko yake  Baraza la Usuluhishi la Ndoa linalotambuliwa kisheria ambapo ni Ofisi ya Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Baraza la Kata, Mabaraza ya Ndoa ya Kidini katika Misikiti
na Makanisa.
2. Baraza litasikiliza malalamiko na likishindwa kusuluhisha, hati maalumu itaandikwa kwenda mahakamani ikielezea mgogoro kwa kifupi na baraza kutoa maoni yake kwa suala husika.
4. Mahakama itasikiliza shauri husika na ikiridhia itatoa tamko la kuvunjika kwa ndoa (decree).
Moja ya basi la Machozi Band linalomilikiwa na Judith Wambura ‘Lady Jaydee.
Tamko la kuvunjika ndoa litawasilishwa Rita kwa ajili ya kusajiliwa na kuingizwa katika daftari la talaka. Baada ya hapo msajili atatoa hati ya talaka ambayo ni uthibitisho wa kuvunjika kwa ndoa na utaratibu wa mgawanyo wa mali utafuata kwa kila kilichochumwa (hata kijiko) wakati watalaka hao wakiwa ndani ya ndoa.
JIDE AFICHA MAWASILIANO YAKE
Risasi Jumamosi lilimsaka Jide kwa njia mbalimbali lakini hakupatikana. Baadhi ya watu wamesema kwa sasa mwanamuziki huyo ameficha mawasiliano yake.
Judith Wambura ‘Lady Jaydee akiwa na aliyekuwa mumewe Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteni.
ALICHOSEMA GARDNER
Gardner alipotafutwa na mwandishi wetu kwanza alianza kwa kukana madai kwa mtindo huu.
Mwandishi: (anajitambulisha kwa jina na kampuni anayofanyia kazi), najua uko kwenye mgogoro wa mali na shemeji (Jide).
Gardner: Kwanza huo mgogoro unaniambia wewe, mimi siujui. Lakini kwa hayo unayotaka kuniuliza nasema no comment (sina cha kusema).

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate