EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, November 13, 2014

URAIA WA WA RWANDA WAMLIZA MISS TZ MPYA!

Na Joseph Ngilisho, Arusha
MREMBO Mariam Mohamed ambaye alishiriki na kushika nafasi ya pili ya Shindano la Miss Mara mwaka 2003, wiki iliyopita alizusha vurumai kubwa kwa kuzichapa kavukavu na mumewe usiku baada ya kumkuta akiwa na baamed ndani ya nyumba moja iliyopo Njiro eneo linalojulikana kama Nguzo Moja jijini Arusha, Amani lina mkanda kamili. 
Mrembo Mariam Mohamed akizichapa kavukavu na mumewe, Rasha Idrisa (38).
Licha ya kuzichapa na mumewe huyo ambaye ni mfanyabiashara aitwaye Rasha Idrisa (38), mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, baamed huyo aitwaye Prisila, naye alipata kipigo kikali toka kwa Miss huyo aliyekuwa akisaidiana kutoa dozi na mpambe wake.
Prissila anayefanya kazi kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Njiro (jina linahifadhiwa) alijaribu kujitetea kuwa hakufahamu kama mpenziwe huyo alikuwa mume wa mtu, alishambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake, ikiwa ni pamoja na kukabwa shingo, hali iliyomuacha hoi na kuapa kutoendelea tena kuiba vya watu.
Operesheni Fichuo Maovu (OFM) ya Global Publishers ilitonywa mapema juu ya kuwepo kwa mpango wa kumfumania Rasha, anayedaiwa kuwa alisafiri kibiashara akimuaga mkewe kuelekea Zambia, tokea Agosti mwaka huu.

Mrembo Mariam Mohamed akizidi kumtaiti mumewe.
Chanzo chetu kinadai kuwa kitu kilichompa mashaka Mariam ni wakati alipokuwa akiwasiliana kwa simu na mumewe, kwani miito yake ilionyesha kuwa mpigiwaji alikuwa nchini. Baada ya kuona hivyo akaanza udadisi wa kujua ni wapi hasa alipo mumewe.
Siku chache zilizopita, chanzo hicho kilisema msichana huyo alipata taarifa kutoka kwa marafiki zake waliopo Arusha, juu ya kuonekana kwa mumewe akila maisha na msichana mmoja mhudumu wa baa, na kwamba alikuwa akitanua naye kila siku na mara nyingi walilala pamoja.
“Mariam amepanga kesho ndiyo aende akawafumanie, kama ni pale baa au wanakoendaga, kwa hiyo nyinyi mnaweza kwenda pale ili mjue kitakachoendelea,” chanzo chetu kiliwasiliana na OFM ambao walifika katika baa anayofanya kazi Prisila bila yeye kufahamu na baadaye Mariam akiwa na mpambe wake nao waliwasili.Baamedi, Prisila akipokea kichapo kutoka kwa rafiki wa Mariam Mohamed kwa kula ujana na mume wa mtu.
Akiwa hatambui kama anafuatiliwa, Prisila pamoja na rafiki yake mmoja ambaye hakufahamika jina lake, waliondoka eneo hilo na kwenda kupanda daladala lililokuwa likielekea Njiro na kuteremka eneo la Nguzo moja. Mariam naye aliondoka na kuchukua usafiri binafsi kwa ajili ya kuwafuatilia wasichana hao huku nyuma yao wakiwa OFM.
Prisila aliingia katika nyumba moja iliyokuwa na geti jeusi majira ya saa tatu na muda mfupi baadaye Mariam na mpambe wake nao waliwasili na kuukuta mlango ukiwa wazi.Baada ya kuingia ndani, waliwakuta wawili hao wakiwa katika mkao wa kimahaba na mara moja Mariam akiwa na fimbo, alianza kumchapa mumewe aliyejaribu kumsihi kwa kupiga magoti ili walimalize jambo hilo kwa mazungumzo. Wakati mume akipigwa na mke, mpambe alikuwa akimpa kichapo cha maana Prisila.
Mume wa mtu na baamedi kwa pamoja wakiwajibishwa kwa kuvunja amri ya sita.
Rasha hata hivyo, baadaye alifanikiwa kumnyang’anya fimbo mkewe huyo na kuanza kutoa vitisho kwa OFM waliokuwa wakipiga picha za tukio hilo. Akizungumza wakati wa sekeseke hilo, Mariam alisema amekuwa akimfumania mumewe mara kwa mara akiwa na wanawake tofauti na mara zote huomba msamaha.
Ingawa hawajafunga ndoa, Mariam alisema alianza kuishi na mwanaume huyo tangu mwaka 2004 na kwamba maisha yao yametawaliwa na migogoro kutokana na ukware wa mumewe.
Kwa upande wake, Rasha alisema yupo tayari kuachana na mkewe ili awe huru na maisha yake.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate