EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, January 27, 2015

DADA AMUUA KAKA YAKE KWA KISU KISA

Stori: Chande Abdallah na Haruni Sanchawa/Uwazi
DUNIA  imekwisha! Binti mmoja mwenye umri wa miaka 19, Rukia Ally anadaiwa kumuua kwa kumchoma kisu kaka yake wa kuzaliwa, Said Ally wote wakati whga Tegeta Mivumoni, Kata ya Wazo jijini Dar es Salaam, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutokana na kijana huyo kutaka kudhibiti tabia zisizofaa za dada yake huyo, tukio lililotokea usiku wa Januari 24 mwaka huu.
Rukia Ally anayedaiwa kumuua kwa kumchoma kisu kaka yake, Said Ally.
Kwa mujibu wa habari kutoka eneo la tukio, inadaiwa kuwa binti huyo alikuwa na kawaida ya kuondoka nyumbani kwao na kwenda kusikojulikana ambako wakati mwingine alikuwa akikaa zaidi ya siku tatu pasipo kurejea nyumbani, huku akiwa hana maelezo ya kutosha.
Inadaiwa kuwa siku hiyo, msichana huyo hakuwa amerudi nyumbani kwa siku tatu, hivyo aliporejea saa tatu usiku, kaka yake alimuuliza alikokuwa, lakini badala ya kumjibu, alimuomba aingie kwanza ndani kwake na kuwa atarejea ili kumpatia majibu.
Mama wa marehemu, Fatuma (katikati) akifarijiwa kwa kumpoteza mwanaye
Aliporejea na kuulizwa swali hilo na kushindwa kutoa majibu ya kueleweka, kaka huyo alimchapa na fimbo mguuni kama ishara ya kumkanya, lakini inadaiwa Rukia alichomoa kisu alichokuwa amekificha nguoni mwake na kumchoma nacho upande  wa kushoto wa kifua chake.
Mama wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Fatuma, alisema binti yake alikuwa na tabia zilizowakwaza ndugu zake, kama kuvaa nguo fupi na kuondoka nyumbani bila kuaga.

Waombolezaji wakiwa msibani.
“Kwa sababu mdogo mtu hakuwa msikivu kwa kaka yake, ndipo kaka mtu akachukua bakora na kumchapa nayo mguuni kwa lengo la kumkanya, ndipo ghafla nikashangaa kumuona Rukia akimchoma kisu kaka yake kifuani na kukichomoa kisha akakimbia na kukitupa kwenye majani.
“Kauli aliyoitoa kaka yake ni kwamba: Mdogo wangu unaniua! Akadondoka hapohapo, nikamkimbilia na kumpakata miguuni mwangu damu zikimtoka mpaka anakata roho nilikuwa nikimtazama,” alisema mama huyo.
Kisu kilichotumiwa kwa mauaji.
Aidha shangazi wa marehemu, Mariam Saidi alidai baada ya Rukia kukimbia, alizungumza naye kwa simu lakini baadaye hakupatikana tena.“Alinipigia nikaongea naye, akasema nimwambie mama yake awadanganye polisi kuwa yeye hakumuua kaka yake, bali alivamiwa na majambazi, nilipomuuliza yupo wapi nikamchukue alisema yupo Ubungo halafu hakupatikana tena,” alisema Mariam.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mivumoni, Deodatus Kamugisha alisema binti huyo alikuwa na tabia ya kutembea usiku na kuvaa nguo fupi kwani kuna siku alikutana naye usiku wa manane akiwa na rafiki yake wakitokea kwenye klabu moja ya usiku.
Marehemu Said Ally enzi za uhai wake.
Taarifa zilizoifikia gazeti hili kutoka kwa mwenyekiti huyo zilidai kuwa Rukia alikamatwa Mkuranga jioni ya Januari 24 akiwa anaelekea mafichoni na amefikishwa kituo cha polisi Wazo Hill kwa ajili ya hatua za kisheria huku mazishi yakifanyika  siku hiyo hiyo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate