EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, January 26, 2015

OFM YAMSHUGHULIKIA WAZIRI WA JK


Stori: Ijumaa Wikienda
Kaa chonjo! Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), mheshimiwa Kassim Majaliwa amejikuta akitumbukia kwenye kamera za Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers baada ya kuchunguzwa kwa kuingia hotelini akiwa ametanguliwa na mrembo mmoja aliyedaiwa kuwa na ahadi naye, Ijumaa Wikienda lina picha kamili.
Gari la mheshimiwa Kassim Majaliwa likiwa eneo la tukio.
OFM ilimshughulikia waziri huyo juzikati kwenye hoteli ya kisasa ya nyota tatu iliyopo maeneo ya Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo mheshimiwa huyo aliingia.

HABARI KAMILI
Majira ya saa 11:05 jioni OFM ilipata taarifa kutoka kwa chanzo chetu kilichopiga simu na kueleza kuwa Waziri Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Dodoma ameingia hotelini hapo akiwa ametanguliwa na mrembo huyo.
Mpambe wa mheshimiwa Kassim Majaliwa akilikagua gari hilo.
“Mimi ni msomaji wenu. Niko hapa hoteli ya....(anaitaja jina). Yule waziri wa JK, anayeitwa Kassim Majaliwa amekuja na gari aina ya Toyota Harrier nyeupe, ameshuka na kuingia hotelini. Lakini dakika kumi kabla kuna mrembo mkali ameingia hapa huku anazungumza na simu, nahisi wana ahadi naye,” kilisema chanzo chetu.
SAA 11:10, OFM YATUA HOTELINI
Kikosi kazi cha OFM kilijikusanya na kuingia ndani ya gari kisha yakakanyagwa mafuta hadi kwenye hoteli hiyo ambapo kilishuhudia gari la mheshimiwa huyo likiwa limeegeshwa.
 ...Akiendelea kulikagua kabla ya kuondoka hotelini hapo.
OFM SAMBAMBA NA GARI
Ili kumtega vyema, OFM waliegesha gari lao kwa kupeana mgongo na la waziri na kusubiri kwa muda huku macho ya kamera yakiangalia kwenye mlango mkubwa wa kuingilia hotelini hapo na wakati mwingine kwenye gari la mheshimiwa.
SAA 11: 22, OFM NDANI YA HOTELI
Baada ya kuona muda unakwenda, mmoja wa watenda kazi wa OFM alitoka kwenye gari na kuzama ndani ambapo alipanda mpaka ghorofani kwa lengo la kuchunguza chochote.
OFM ilibahatika kukutana na mhudumu mmoja ambaye alisema hajamuona mheshimiwa huyo, akamshauri kwenda kujaribu kumuangalia upande wa baa, jambo ambalo kachero huyo wa OFM alilifanya.
Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipanda kwenye gari hilo.
SAA 11: 26, OFM, WAZIRI MACHO KWA MACHO
Kachero wa OFM alitembea hadi kwenye baa ya hoteli hiyo na kukutana na mheshimiwa ana kwa ana (lakini hawafahamiani).Waziri huyo alikuwa amekaa na wanaume wengine wanne wakizungumza. Mazungumzo yao yaliashiria yana msisitizo kama si umuhimu kwa wote.
SAA 11: 30, OFM ARUDI KUTEGA GARINI
Hata hivyo, OFM hakukubaliana na kumkuta mheshimiwa huyo amekaa na wanaume wenzake, alirudi ndani ya gari na kuwapa taarifa wenzake ambao katika kujiongeza walikubaliana kutulia ndani ya gari hadi kuona mwisho wake.
JUA LAANZA KUPOTEZA NURU
Saa 11: 43, jua lilianza kupoteza nuru yake kuashiria kwamba, mchana unakatika na giza linakaribia kupiga hodi.
WAZIRI HUYOOO!
Ilikuwa saa 11:47, ghafla Waziri Majaliwa alitoka hotelini hapo akiwa ameongozana na mwanaume mmoja ambaye OFM hawakuweza kumjua ni nani!
Mheshimiwa Kassim Majaliwa akiwa kazini.
Mheshimiwa huyo alikwenda upande wa dereva lakini kabla hajaingia, mwenzake alilizunguka gari na kuinama kuchungulia chini kukagua usalama. Baada ya kujiridhisha, waliingia wote ndani ya gari na kuondoka zao.
ALISTAHILI KUJIENDESHA?
Baada ya mheshimiwa kuondoka, OFM walijiuliza kama ni halali kwa waziri kujiendesha mwenyewe badala ya dereva ambaye kila waziri hupewa na serikali.
Ili kutaka kujua hilo, OFM walimtwangia simu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, mheshimiwa Hawa Ghasia na kumuuliza kama ni sahihi kwa waziri kuendesha gari mwenyewe.
“Kama waziri ana safari zake binafsi na si muda wa kazi hakuna shida. Hata kama ni muda wa kazi anaweza kujiendesha mwenyewe lakini kwa gari binafsi siyo la serikali,” alisema mheshimiwa Ghasia.
PONGEZI WAZIRI MAJALIWA
OFM imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kufichua maovu katika jamii ya Tanzania. Hivyo, kama kweli Waziri Majaliwa agekuwa ameingia na kimwana kwenye hoteli hiyo lazima OFM wangemnasa tu. Lakini alionesha mkubwa. Kwa sababu hiyo, Ijumaa Wikienda linammwagia pongezi kibao.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate