EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, February 18, 2015

BARUA NZITO STARA THOMAS JITATHMINI UPYA

KWAKO mwanamuziki wa Injili na Bongo Fleva, Stara Thomas. Bila shaka ni mzima wa afya na unaendelea na mishimishe zako maana najua una mambo mengi, muziki wa kidunia na ule wa kiroho.
Binafsi ni mzima. Naendelea na majukumu yangu kama kawaida. Nimekukumbuka kwa barua leo maana ni muda mrefu hatujaonana. Sikulaumu maana mjini mipango kama alivyoimba Mwanamuziki Ali Chocky wa Extra Bongo.
Dhumuni la barua hii kwanza kabisa ni kukupa pole kwa tukio lililotokea juzikati maana suala la kukutwa na mwanaume mwingine tofauti na mumeo, kila mmoja analijua uzito wake.

Hakuna anayeweza kulifurahia, nina imani hata wewe lilikufedhehesha sana lakini hakukuwa na namna, ili mambo yaende lazima matukio kama hayo yatokee, maisha yaendelee pia iwe fundisho kwa wengine.
Sambamba na kukupa pole, bado nina neno nataka kukupa. Sikufurahishwa na tukio lile. Niwe mkweli kwamba kilichonifanya nisifurahi ni kwa sababu wewe nakuheshimu.
Nilipoona umeingia katika skendo ile moyoni nikasema: “Vipi kwa wale ambao siwaheshimu, watakuwa wachafu kiasi gani?”
Sikia dada yangu, kitendo kile hakikuwa cha kiungwana. Heshima yako ni kubwa sana katika jamii hivyo unapaswa kila unachokifanya uwe makini. Mbali na kuwa mtu maarufu lakini wewe ni mama wa familia, tena watoto wakubwa tu.
Kwa umri ulionao ukiingia katika skendo kama hiyo, ni aibu kwa wanao. Si tu kwa wanao, kuna ishu ya waimbaji Injili wenzako ambao walikuwa wanatambua mchango wako mkubwa.
Lazima waimbaji hao watakuwa wamesononeka sana. Utakuwa umewavunja nguvu, hata wale ambao walikuwa wanapenda kazi zako, naamini pia utakuwa umewakatisha tamaa.
Walikuwa wakitegemea wewe ambaye unawabadilisha tabia kupitia nyimbo zako za Bongo Fleva na Injili uwe kioo cha tabia njema lakini badala yake wanakuona umeangukia kwenye kashfa ya kukutwa na mchepuko.
Mbali na tukio hilo, baadhi ya matukio yako ya nyuma ambayo mengi yalikuwa hayaripotiwi, yanaonesha kuna walakini kama kweli wewe ni kioo cha jamii.
Unapaswa kujitathmini upya. Unapaswa kuangalia upya njia zako ili uweze kuona sababu za kubadilika na kuwa mtu mwema. Naamini unaweza, hakuna mwanadamu aliyemkamilifu.
Wengi tunakosea, tunaamka na kuanza upya safari. Safisha njia zako, kwa imani tunaami ukitubu dhambi, Mungu pia anasamehe na hakika utakuwa mpya.
Huna sababu ya kusononeka moyoni, chukulia kama changamoto ya maisha. Wapo wengi wana matukio mazito kuliko hata hilo la kwako lakini hayaonekani hadharani kwa sababu siyo watu maarufu.
Naamini utakuwa umenielewa, Mungu awe pamoja na wewe, nakutakia mafanikio zaidi na uendelee kumtumikia Mungu wetu kwa nyimbo zako!
Kwa leo ni hayo tu! 

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate