EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, February 23, 2015

CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI CHATOA TAMKO KUHUSU SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 ILIYOZINDULIWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE FEBRUARI 13, 2015‏


 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Zanzibar, Musa Kombo Musa (kulia), akimkaribisha Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, James Mbatia (katikati), ili azungumze na wanahabari Dar es Salaam jana asubuhi wakati akitoa tamko hilo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosene Nyambabe.
 Mwenyekiti  wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Taifa, James Mbatia (kulia), akionesha kitabu cha Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana asubuhi, wakati akitoa tamko la chama hicho juu sera hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosene Nyambabe na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Musa Kombo Musa.
 Hapa mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Wanahabari wakiwa katika mkutano huo.
Wajumbe wa Halmshauri Kuu (NEC) ya chama hicho waliokuwepo kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Honest Mombory, Katibu wa Wazee, Ernest Mwasada, Dk.Nderakindo Kessy ambaye pia pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Angelina Mutahiwa na Esther Komba.

Dotto Mwaibale
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia amesema kuwa uzinduzi wa Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 ni mpango wa serikali kuwalaghai wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu utakao fanyika Oktoba mwaka huu.

Pia amesema hali ya elimu nchini ni kama mgonjwa aliyekuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, hivyo serikali isiwe inatoa majibu mepesi kwenye masuala magumu ambayo yanagusa maisha ya watanzania.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akitoa tamko la chama hicho kuhusu sera hiyo Mbatia  alisema kuwa mnamo Januari 31 na Februari mosi mwaka 2013, aliwasilisha hoja bungeni kuhusu udhaifu uliopo katika sekta ya elimu.

Alisema kuwa aliorodhesha athari mbalimbali za udhaifu wa wa elimu itolewayo nchini lakini suala hilo lilionekana kutawaliwa na siasa ambapo haikuwa lengo lake,lengo lilikuwa kuhakikisha kuwa sera mbalimbazi za elimu zinaboreshwa.

Mbatia aliongeza kuwa mnamo Februari 13, 2015 mwaka huu Rais Jakaya Kikwete, alizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 lakini ikiwa haijajibu hoja alizokuwa amezitoa.

Alifafanua kuwa wakati Rais akihutubia alisema kuwa sera hiyo ilitumia miaka saba kukamilika, lakini Mwenyekiti huyo alisema baada ya kuipitia alibaini sera hiyo kuwa na lugha ngumu huku ikiwa na makosa mengine mengi.

Mbatia alisema anachokiona kwa serikali kuzindua sera hiyo mwaka huu ni mikakati ya kuelekea uchaguzi mkuu,kwani yaliyomo ndani ya sera hiyo yamelenga kuwalaghai wapiga kura.

Aidha alisema mambo hayo ni pamoja na kutangaza kuwa elimu ya msingi kutolewa bure bila karo na lugha iliyotumika inawachanganya watanzania hivyo ni vigumu kwa wananchi wa vijijini ambao wengi wao hawana elimu kutambua yaliyoandikwa ndani ya sera hiyo.

"Mfano sera mpya ina matamko mawili ambayo  inawachanganya watanzania kuhusu lugha ya kufundishia,moja inatamka Kiswahili kitatumika kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu,na ya pili inatamka kuwa Kingereza kitatumka kama lugha ya kufundishia katikan ngazi zote za elimu.

"Matamko haya mawili, kwanza yanakwepa lawama zinazotokana na malumbano ya muda mrefu kuhusiana na lugha gani inafaa kufundishia, pili imehalalisha mifumo miwili ya elimu ndani ya nchi moja" alisema Mbatia kwa msisitizo

Hivyo alisema serikali ilipaswa kutengeneza sera ambayo inazungumza kwa uhakika kuhusu suala la lugha ya kufundishia, kuliko kutoa tamko la sera lisilo na msimamo.

Aliweka wazi kuwa wanapendekeza iundwe tume ya kudumu ya elimu nchini itakayoshughulikia pamoja na mambo mengine kuhakikisha ubora wa elimu unapatikana nchini.

Vilevile alisema wanaiomba serikali kupitia upya sera hiyo kabla haijaanza kutumika ili kuepusha taifa na madhara ambayo yameonesha dalili za kutokea hata kabla haijaanza kutumiaka.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate