EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, February 16, 2015

HAKUNA KAMA CHRISTIAN BELLA

Na Waandishi Wetu/Ijumaa Wikienda
Wikiendi iliyopita, dunia nzima ilikuwa ikiadhimisha siku ya Valentine’s Day au kwa Kiswahili Siku ya Wapendanao! Mambo yalinoga ndani ya Ukumbi wa Dar Live ambapo wakali wa mapenzi, Christian Bella ‘Obama’ na Mzee Yusuf walifanya yao na kuzikonga vilivyo nyoyo za maelfu ya mashabiki waliofurika, Ijumaa Wikienda lilikuwepo kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
Mkali wa mapenzi, Christian Bella ‘Obama’ akikonga nyoyo za mashabiki katika usiku wa siku ya Valentine’s Day.
BURUDANI YAANZA
Pazia la burudani lilifunguliwa na Bendi ya Malaika Music ambapo waliimba na kucheza muziki kwa staili ya kikongomani, wakazikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliohudhuria kabla ya kiongozi wao, Christian Bella kupanda jukwaani na wimbo wake wa Usilie, shangwe zikaibuka kutoka kila kona ya ukumbi huo.
Ukumbi wa Dar Live ulifurika mashabiki wengi katika siku hiyo ya wapendanao.
NANI KAMA BELLA?
Bella akiwa jukwaani, alianza kwa kutambulisha bendi yake mpya ya Malaika kisha burudani ikaendelea ambapo alitambulisha wimbo wake mpya uitwao Nashindwa ambao ulipokelewa kwa shangwe za nguvu na maelfu ya mashabiki waliodhuria shoo hiyo ya kipekee.
Burudani ziliendelea ambapo Bella alikamua wimbo wake mwingine wa Msaliti, ukumbi mzima ukafurika kwa shangwe za nguvu, akaendelea kukamua nyimbo zake nyingine na mwisho, akawaomba mabaunsa waliokuwa wakilinda usalama katika ukumbi huo wa kisasa, kuwaruhusu akina mama kupanda jukwaani kwa ajili ya kuimba naye wimbo wa Nani Kama Mama.
Mkali mwingine wa mapenzi Mzee Yusuph akifanya yake stejini.
Ni hapo ndipo umashuhuri wa Bella ulipoonekana kwani akina mama na wasichana kinbao walipanda jukwaani na kuanza kuimba pamoja Wimbo wa Nani kama Mama, shangwe za nguvu zikatawala jukwaani hapo na kuweka historia ambao haijawahi kutokea huku wengi wakilizwa na wimbo huo kutokana na ujumbe uliomo ndani yake.

Wakati watu wengine wakiimba ‘nani kama mama’, nyomi nyingine ilikuwa ikibadilisha maneno na kuimba ‘nani kama Bella’ kuthibitisha kwamba hakuna msanii anayeweza kumfikia katika suala zima la burudani.
Huko Msasani Club pia mambo yalikuwa moto moto.
Baada ya kukamua sana, Bella pia alikumbushia enzi za zamani alipokuwa na Akudo Impact kwa kuimba wimbo wa Bomoabomoa ambao nao uliziguza hisia za wengi, akashuka jukwaani huku mashabiki wakionekana kuwa na hamu kubwa ya kuendelea kusikiliza nyimbo zake.
Mwandishi wetu alimfuata Bella na kuzungumza naye mawili matatu:
Mwandishi: Shoo yako imekubalika sana, watu wamecheza na kufurahi mno, unalizungumziaje hili?
Bella: Muziki ndiyo kazi yangu, nimekuja kufanya kazi kwa hiyo nikiona mashabiki wanakubali kazi zangu, nafurahi sana.
Mwandishi: Unafikiri kuna msanii gani wa kushinada na wewe?
Bella: Mimi sijaja kushindana na mtu yeyote ila nimekuja kuwapa mashabiki wangu ile kitu wanataka. Nataka waupende muziki wangu.
MZEE YUSUF ACHA KABISA
Baada ya Bella kushuka jukwaani, iliwadia zamu ya mfalme wa muziki wa mwambao Bongo, Mzee Yusuf ambaye naye alifanya shoo ya nguvu na kuweka historia ya aina yake akiwa na Bendi ya Jahazi Modern Taarab. Nyimbo zao kibao za mapenzi zilishangiliwa kwa nguvu mpaka usiku mnene.
MSASANI CLUB NAKO KULIPENDEZA
Wakati huohuo, burudani nyingine ya nguvu ilikuwa ikiendelea katika Ukumbi wa Msasani Club jijini Dar es Salaam ambapo wasanii lukuki walikuwa wakikamua shoo ya nguvu wakiwemo Msaga Sumu ambaye alikamua nyimbo zake kibao ukiwemo Shabiki wa Yanga ulioshangiliwa kwa nguvu, hasa ukizingatia kuwa timu hiyo ilikuwa imepata ushindi kwa kuifunga BDF XI FC ya Botswana kwa mabao 2-0.
Burudani iliendelea kwenye ukumbi huo ambapo baada ya Msaga Sumu kushuka, timu ya Radio EFM ikiongozwa na DJ Majay na Sebo ilipanda jukwaani kabla ya kumpisha mamaa wa majanga, Snura kufanya yake. Baada ya Snura alipanda Recho ambaye alizua gumzo kwa kuvaa kinguo kifupi kilichoacha wasi sehemu kubwa ya maungo yake.
Alipotaka mtu mmoja apande kucheza naye jukwaani, njembammoja ambaye hakufahamika jina lake, alipanda na kuanza kumbeba juujuu msanii huyo na kusababisha mashabiki waanze kumwagia pombe njemba huyo nakumtaka amuache Recho aendelee kutumbuiza.
Burudani ziliendelea ambapo mpaka Ijumaa Wikienda linaondoka ukumbini hapo, shangwe zilikuwa zinaendelea kutawala.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate