EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, February 17, 2015

MAPIGANO NA MAGAIDI TANGA HII NDIYO FULL STORY


Na Mwandishi Wetu, Tanga
NI kama kumekucha! Siku chache tu baada ya Gazeti la Ijumaa (ndugu na hili) kuandika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; Kiongozi wa kikundi cha kigaidi kinachoua polisi na kuiba silaha kwenye vituo nchini...NI HUYU, kundi jingine limeibuka na kuandika mkanda wa video wakizungumzia uhalifu.
Moja ya kikosi cha kigaida cha Al Shabaab.
Cha ajabu, sanjari na kundi hilo linalodai liko Tanga, Tanga hukohuko kwenye Kitongoji cha Amboni, Ijumaa iliyopita kulizuka mapigano kati ya polisi, askari wa JWTZ wakipambana na kundi lililodhaniwa ni la kigaidi likiwa limepiga makazi ndani ya mapango ya kihistoria ya  Amboni, Uwazi lina full story.
Katika mapigano hayo hadi juzi Jumapili, askari mmoja wa JWTZ aliuawa huku wanajeshi watatu na askari polisi wawili wakijeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo.

MASHUHUDA WA MAPIGANO
Kabla Uwazi halijatiririka na video hiyo, lilizungumza na wananchi wenye makazi yao kwenye Kitongoji cha Amboni ambako mapigano ya askari na wahalifu yalitokea.
Mzee Ibrahimu Ally, yeye anasema: “Siku ya tukio (Ijumaa asubuhi) mimi nilikuwa nimepumzika ndani kwangu lakini ghafla nikasikia mlio wa risasi kama mara mbili hivi.
“Mke wangu alikuwa anafua, akaja mbio ndani akisema ni majambazi. Nilimwambia funga mlango haraka sana, akaufunga. Lakini cha ajabu milio ya risasi ikawa inaongezeka kadiri muda ulivyokwenda.
“Ilifika mahali nikajua si majambazi bali tumevamiwa na majeshi ya nje ya nchi. Kwani sasa risasi zilikuwa zikirindima kila muda. Hali ikawa tete kwa kweli. Hata hapa ninapoongea na wewe siamini kama ile milio ya risasi haitajirudia tena.” 
Kundi la wahalifu wanaodaiwa kujificha na kushambulia Polisi katika mapango ya Amboni.
WAZIKIMBIA NYUMBA
Mwanahawa Mudale yeye alisema: “Ilibidi tuhame majumba kwenda kujificha, tatizo ni ile milio ya mabomu na risasi na baadaye tukaona chopa (helikopta) ikitembea angani. Awali tulijua ni vita ya nchi na nchi, kumbe walikuwa askari wetu.”
SIKU MBILI HAKUNA KULALA
Baadhi ya mashuhuda wanasema kutokana na milio ya risasi kwa siku ya Ijumaa hadi Jumamosi asubuhi, hakuna mwananchi aliyepata usingizi.
“Mimi na familia yangu hatujalala jamani. Risasi na mabomu yasikieni hivihivi tu. Kuna wakati tulikuwa tukiona miale ya moto kutokea kwenye eneo la mapango. Wakati mwingine badala ya moto tuliona moshi mkubwa.
“Kumbe wanajeshi wetu nao walishafika kupambana na hao watu,” alisema Simeon Patrick, mkazi wa Kitongoji cha Karasha, Amboni.
INAVYODAIWA
Habari zilizosambaa juzi, zinadaiwa kundi hilo lililopambana na askari ni la kigaidi ambapo safari yao kubwa ilikuwa kwenda kufanya ugaidi wa kumwaga damu nchi jirani ya Kenya.
Moja ya dhana ya kivita ya Polisi ikiwa kazini kubambana na matukio ya uhalifu.
Wale jamaa nasikia walikuwa wakipeleka vifaa nchini Kenya eneo la mwambao ili waje wafanye uhalifu baadaye.
“Sasa wakiwa katika hatua za mwisho mwisho baada ya kupeleka silaha za kivita, wakashtukiwa. Ikabidi waache silala zao eneo walipozificha na wao waje Tanga kujificha kwenye mapango.
“Lengo lao, watulie mpaka hali kule Kenya itakapokuwa imepoa ndipo wajitokeze. Sasa kilichotokea ni kwamba, wakati wanaishi mapangoni ilibidi waanze kutoka kutafuta chakula kwa kufanya uhalifu mdogomdogo ndipo siku moja jamaa yao mmoja akakamatwa kwa uhalifu.
“Yule jamaa ndiye aliyewapeleka polisi walipo wenzake na kutokea kwa mapigano makali kama yale,” alisema mtoa habari mmoja huku akiomba jina lake lihifadhiwe.
WANACHOAMINI WANANCHI, TOFAUTI NA POLISI
Uwazi lilibahatika kuzungumza na baadhi ya wananchi wa jijini Tanga ambapo karibu wote walikuwa na mtazamo mmoja tu.
“Kutuambia wale ni majambazi si sawasawa. Majambazi wetu tunawajua, polisi wanawatosha sana, sasa hawa wametokea wapi mpaka JWTZ washirikishwe?” alihoji Paulina Mathias, mkazi wa Chumbageni, Tanga.
Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja.
Kusema ukweli serikali ituambie moja. Lakini wale si majambazi. Kwanza mpaka leo hii (juzi) hawajamkamata hata mmoja zaidi ya kujeruhi askari wetu na kumuua mmoja. Wale ni magaidi, lazima tuwe makini sana,” alisema Ally, mkazi wa Duga Maforoni, Tanga.
KUHUSU VIDEO MPYA
Tukiachana na mapigano ya Amboni, sasa turudi kwenye video mpya ya watu waliojiita ni watetezi wa haki dhidi ya udhalimu.
Video hii ipo ndani ya mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wanaonekana watu wawili wakiwa wamevaa mavazi ya kininja ili wasijulikane.
Watu hao wanasema wanapinga jamii yao kukamatwa na kuuawa mara kwa mara wakidai jeshi linawaonea hivyo kutangaza kupambana na askari.
Video hiyo haipishani sana na ile iliyotangulia kuandikwa kwenye gazeti ndugu na hili la Ijumaa.
KAULI YA JESHI LA POLISI
Akizungumza na Uwazi jijini Tanga muda mfupi baada ya kutulia kwa mapambano ya Amboni, Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja aliwataka wananchi kutulia na kuendelea na shughuli zao za kawaida huku akisisitiza:
“Askari walifika mapangoni, kundi lile ni la majambazi. Lilianza kufanya mashambulizi ya risasi na katika majibizano,  askari sita walijeruhiwa na kuwahishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo,” amesema Kamishna Chagonja.    
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate