EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, February 19, 2015

MASTAA WAMCHANA DIAMOND

IMEKULA kwake! Wasanii wa sinema na Bongo Fleva wamemchana vibaya staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba si mtokaji kwenye misiba ya wenzake.
Staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Wakizungumza na Amani kwenye maziko ya baba mzazi wa Mbongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, Ebby Sykes, Jumatatu iliyopita, wasanii hao walioomba majina yao yalindwe walisema kumbukumbu za vichwani mwao zinaonesha kuwa, Diamond amekuwa akichagua misiba ya kujitokeza hasa ile ambayo itampa  ‘kavareji’ kwenye vyombo vya habari.

WASIKIE WENYEWE
“Mimi nakumbuka wakati wa kifo cha Kanumba (Steven), Diamond alitokea kwa sababu ulikuwa msiba mkubwa sana na kweli alipata kavareji ya kutosha kwenye media.
“Halafu akaonekana tena kwenye msiba wa baba yake Wema Sepetu, nadhani kwa vile alikuwa mtu wake Wema wakati huo asingeacha kwenda. Lakini baada ya hapo sikumbuki,” alisema msanii mmoja.
Msanii mwingine aliongeza: “Halafu Diamond na Dully ni washikaji, sasa jamaa tunasikia yuko Zenji tu hapo anakula bata na Zari (Zarina Hassan) lakini ameshindwa kuja Dar kumzika baba mzazi wa mshikaji  wake.”
Akaongeza tena: “Kama sijasahau hata kwenye kifo cha mwanamuziki wa Bendi ya Msondo, marehemu Maalim Gurumo hakutokea japokuwa alikuwa amerudi nchini kutoka nje. Magazeti mliandika kwamba Wema alimzuia kwenda kuzika. Sasa ni vizuri kweli?”
WANAOTOA POLE KWENYE MITANDAO
Wakati wasanii hao wakimchana Diamond, wasanii wa filamu, Tamrina Poshi ‘Amanda’, Isabela Mpanda ‘Bela’ na Baby Madaha wao walisema wanakerwa na tabia ya baadhi ya wasanii kutohudhuria misiba ya wenzao na kuishia kutoa pole kwenye mitandao ya kijamii.
Wakizungumza na Amani, wasanii hao walisema imekuwa ni kawaida kwa wasanii kutohudhuria misibani bila kuwa na sababu na kuongeza kuwa tabia hiyo si nzuri kwa umoja wao.
AMANDA
AMANDA
“Mfano mzuri tunauona hapa leo, mwenzetu kafiwa na baba yake ukiangalia wasanii waliohudhuria wanahesabika lakini nimepata mshangao kwa sababu rafiki mkubwa wa Dully ni Diamond lakini hapa hajaonekana. Tunaona tu pole zinaishia kwenye mitandao. Mtu yupo Zanzibar tu hapo na anatupia picha akiwa na mpenzi.”
BELA NAYE
Kwa upande wake, Bela alisema alipata taarifa za msiba huo akiwa hospitali amelazwa lakini akaona ni vema ahudhurie mazishi kwa kuomba ruhusa kwa daktari pamoja na kuwa hali yake haikuwa nzuri.
“Nilikuwa nimelazwa na niliwekewa dripu kabisa baada ya kugundulika nina malaria tano, lakini nikaona siwezi kukosa kuhudhuria msiba kwa sababu marehemu mzee Sykes mbali ya kuwa baba yetu alikuwa mshikaji wetu sisi wasanii,” alisema Bela.
BABY MADAHA.
BABY MADAHA
“Jamani hili jambo lisikieni tu kwa watu, mimi sikuamini kwa sababu siku siyo nyingi Dully aliniambia baba yake anaumwa miguu  na walikuwa kwenye mipango ya kumpeleka India akatibiwe, kumbe baadaye hali ilibadilika mpaka umauti ukamkuta, nimeumia sana.
“Wasanii tuache ‘u-snich’ (unafiki) kwa sababu wengi wetu wanaishia kuandika kwenye mitandao tu mi sidhani kama hiyo ni faraja, faraja ni kumfariji mwenzetu tena kwa ukaribu.”Diamond alipotafutwa kwa njia ya simu alisema: “Hata mimi nimeumia kwa kifo cha baba’ke Dully lakini si kwamba sijakwenda makusudi, nilikuwa na dharura.”
Mzee Sykes (pichani) alifariki dunia, Jumapili ya Februari 15  katika Hospitali ya Muhimbili ambapo alikuwa akisumbuliwa na presha. Alizikwa Februari 16 katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate