Na MatukiodaimaBLOG
CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kimepata pigo kubwa kufuatia kifo cha aliyekuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya wilaya hiyo (NEC) Bi Elizabeth Haule.
Mbali ya kuwa MNEC wa wilaya hiyo Haule pia alikuwa ni mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Ludewa kabla ya kujiuzulu kwake mwezi February mwaka jana baada ya kuchaguliwa nafasi hiyo ya NEC na nafasi hiyo kuwa wazi hadi sasa.
katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Ludewa Felix Haule alisema kuwa kifo cha kionozi huyo kimetokea usiku wa kuamkia leo akiwa katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa ambako alilazwa jana mchana kwa tatizo la moyo.
Bw Haule alisema kuwa siku ya jumatatu wiki iliyopita marehemu alipata kuongoza kikao chake cha mwisho cha baraza la vijana la wilaya ya Ludewa na baada ya hapo hali yake ya afya ilianza kuzidi kuwa mbaya zaidi kabla ya kuamua jana kwenda Hospitali ambako walimlaza
Alisema kuwa mazishi ya mjumbe huyo wa NEC wilaya ya Ludewa yanataraji kufanyika kesho kutwa jumamosi kijijini kwake Mholo kata ya Luana wilayani Ludewa .
Aliyekuwa MNEC wa wilaya ya Ludewa Elizabeth Haule (kulia) akishiriki na vijana wenzake kuigiza |
Marehemu Elizabeth Haule enzi za uhai wake |
Hivyo alisema kuwa kifo cha MNEC huyo kimekuja huku wilaya ya Ludewa ikiwa katika maandalizi ya kuanzimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM sherehe iliyopangwa kufanyika siku ya jumapili ya February 8 mwaka huu kwa mara ya kwanza katika kata ya Kilondo mwambao mwa ziwa nyasa lakini kutokana na msiba huo mkubwa sherehe hizo zitasogezwa mbele hadi Februari 15 mwaka huu.
" Mimi pia nilikuwa nikijiandaa kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea wilayani Ludewa katika sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM kama mgeni rasmi ila sitaweza kufanya hivyo na chama kimeamua kusogeza sherehe hizo hadi jumapili ya ijayo ili kupisha maombolezo kwa wana CCM kwa kifo cha kiongozi huyo"
No comments:
Post a Comment