EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, February 20, 2015

TOP 10 YA WAIGIZAJI WA KIKE WENYE MVUTO AFRIKA!

Tasnia ya filamu Afrika inakuwa kila siku kiasi kwamba zile ndoto za kufanya kama wenzetu wa Hollywood (Marekani) na Bollywood (India) huenda siku moja zikatimia.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kama ilivyo Hollywood na kwingine kwenye waigizaji wa kike wenye mvuto, wapo pia waigizaji wa kike Afrika ambao ni ‘visu’.Leo hii ikihitajika Top 10, kila mmoja atakuwa na yake lakini mtandao wa  umefanya kazi ya kuorodhesha waigizaji 10 wa kike wenye mvuto kama ifuatavyo;
10. Elizabeth Michael ‘Lulu’
Binti huyu ana umri wa miaka 21 lakini ni mrembo na anayejiamini. Ni binti kutoka Tanzania mwenye kipaji cha kuigiza kiasi cha kuwa tishio kwa wakongwe. Ni kweli huwa anatumia ‘make up’ lakini hata akiwa hajatumia wala kuvaa ‘mawig’, bado anaonekana ni mwenye kuvutia.
9. Omotola Jalade Ekeinde.
Ni mmoja wa mastaa wa kike nchini Nigeria mwenye mvuto wa aina yake. Kwa sasa ana umri wa miaka 37 na watoto wanne lakini bado anaonekana mrembo kiasi cha baadhi ya mashabiki wake kumuita Omosexy.Kutokana na kipaji alicho nacho, amejikuta akiwa na mashabiki wengi katika Bara la Africa na kwingineko duniani. Mbali na uigizaji pia ni mwanamitindo na mwananamuziki.
8. Chinyere Yvone Okoro
Huyu ni muigizaji anayetokea nchini Ghana. Katika orodha ya waigizaji wa kike waliomo nchini humo, mrembo huyu amebaki kuwa tishio na imemfanya kuingia katika orodha hii ya wasanii wa kike wakali Afrika.
7. Jackline Wolper.
Huyu ni muigizaji kutoka Tanzania mwenye mvuto wa aina yake. Kwa mujibu wa maelezo yake, uzuri alionao unatokana na mfumo mzuri wa kula aliojiwekea. Anakula sana mbogamboga, matunda na maji mengi, hali inayomfanya autunze urembo alionao.
6. Genevieve Nnaji.
Ana umri wa miaka 36, anatokea Nigeria. Mwanadada huyu anatajwa kuwa na mvuto wa aina yake kiasi cha kupata usumbufu kutoka kwa wanaume kibao.Ameigiza filamu nyingi na zote amezitendea haki kutokana na namna anavyouvaa uhusika.
5. Jackie Appiah Agyemang.
Amezaliwa miaka 32 nchini Canada lakini amekulia nchini Ghana. Ni binti mrembo na mwenye kipaji ambaye aonekanapo kwenye televisheni, huthibitisha kwamba kuna kitu cha ziada alichojaaliwa na Mungu.
4. Nadia Buari.
 Huyu ni msanii kutoka Ghana aliyezaliwa miaka 30 iliyopita. Licha ya umri kusogea, hachuji kwa uzuri. Amecheza filamu nyingi na kadiri siku zinavyokwenda ndivyo anavyozidi kuwa tishio kwenye tasnia ya uigizaji.
3. Ini Edo.
Hivi unaanzaanzaje kumuacha mrembo huyu pale unapotaja medemu wakali kwenye tasnia ya filamu Afrika? Naamini huwezi, labda uwe na chuki zako binafsi.Ana umri wa miaka 31 na ana uzuri wa asili unaomfanya atumike kwenye filamu nyingi za Nigeria.
2. Stephanie Okereke Linus.
Huyu ni binti kutoka Nigeria ambaye wengi wanamtaja kuwa muigizaji mwenye mvuto kuliko wote Afrika. Ana miaka 33, aliwahi kushiriki mashindano ya urembo nchini Nigeria na kuibuka mshindi. Kuanzia hapo amekuwa gumzo kwa uzuri wake na amekuwa akitumika sana kwenye filamu nyingi.
1.Rita Dominic.
Wafuatiliaji wa filamu za Nigeria watakuwa wanamjua vizuri binti huyu. Ana miaka 40 lakini bado anadai. Kila sehemu ya mwili wake ina muonekana wa kiurembo.
Angalia midomo yake, angalia macho na ngozi yake. Hakika ni kati ya waigizaji wa kike Afrika wenye mvuto wa aina yake.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate