EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, February 18, 2015

“WOMEN MAKE IT HAPPEN” - EVENT


Siku Ya Wanawake Dunia huadhimishwa kila ifikapo Tarehe 8, mwezi wa tatu. Siku hii huadhimishwa kwa shughuli mbalimbali na kutambua mchango wa mwanamke katika maendeleo ya Jamii.
Mwaka huu kitaifa Siku hii itaadhimishwa mkoani Morogoro lakini kampuni ya TruMark ya mjini Dar es Salaam imeandaa warsha maalum katika maadhimisho hayo ambayo itafanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam Machi 7 mwaka huu.Kauli mbiu ya Siku hii ni Women Make It Happen’ ikiwa inamaanisha wanawake wanafanikisha.
TruMark imeamua kufanya tamasha hili, baada ya uzoefu tulioupata katika shughuli zetu za mafunzo ambazo tunatoa kwa watu mbalimbali, tulioana kuna changamoto mbalimbali ambazo wanawake wanazipata.

Hii likafanya tuone kuwa Siku Ya Wanawake ni jukwaa ambalo linaweza kukutanisha wanawake katika kada mbalimbali na kuzungumza mambo yao katika kujikwamua kiuchumi na kujifunza kwa wengine ambao walipitia changamoto hizo lakini leo hii wameweza kufika mbali baada ya kupambana.
TruMark imepata Baraka zote kutoka Wizara ya Wanawake Jinsia na Watoto katika kuandaa siku hii muhimu. Kwenye maadhimisho haya, kutakuwa na mada ambazo zitatolewa na wanawake kutoka katika kada tofauti, juu ya uongozi, biashara na uchumi, ujasiriamali.
Lakini pamoja  na elimu ambayo itatolewa kutakuwepo na burudani pia kutoka kwa wasanii wanawake maarufu na chipukizi nchini ambao wataungana na wanawake wengine kusheherekea siku yao hii.
Wanawake wanakaribishwa kushiriki katika siku hii ili kuweza kupata elimu ambayo itawasaidia kwenye shughuli zao za kila siku. Kwa upande mwingine tunatoa wito kwa wadhamini kujitokeza ili kufanikisha siku  hii kwani mama ndiye kiungo cha familia.
Na kama ijulikanavyo kuwa katika kila mwanaume mwenye mafaniko basi nyuma yake yuko mwanamke shupavu.
Trumark tunawakaribisha wadau na wahisani kutoa ufadhili. Mchango wowote utatambulika katika kufanikisha tamasha la wanawake litakalowawezesha walengwa ambao ni wanawake kufikia malengo yao kwa kutumia changamoto na kuzibadili  kuwa fursa.
Asilimia 10 ya mapato yatakayopatikana kwenye tamasha hili yatakwenda kusaidia wasichana kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi. Wasichana hawa watatokana na shule tutakayoichagua.
Kuhusu TruMark hii ni kampuni inayojihusisha na utoaji mafunzo mbalimbali ya uongozi, biashara na ujasiriamali yenye lengo ya kuboresha ufanisi kwa matabaka mbalimbali katika jamii.
MWISHO.
Agnes Mgongo
Managing Director
TruMark
Human Potential Skills Development
Josam House Complex -Mikocheni
P.Box 12382- Dar es Salaam
Mobile:  +255 754 095 017 / 658 095017
Email: amgongo@trumark.co.tz
Website: www.trumark.co.tz

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate