EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, March 12, 2015

MWANAMKE DAR AJIFUNGUA CHATU!


WAANDISHI WETU/Amani
MAAJABU! Ama kweli dunia ina mambo na ya Mungu mengi! Mwanamke mmoja, mkazi wa Mbezi- Maua jijini Dar aliyefahamika kwa jina moja la Neema, amelea ujauzito wake kwa miezi tisa yenye matumaini lakini siku ya kujifungua akaambulia kiumbe cha ajabu kilichofanana na nyoka aina ya chatu, Amani limeifuatilia habari hii kwa kina.
Neema anayedaiwa kujifungua Chatu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, awali Neema alikuwa akisumbuliwa na pepo wachafu hali iliyomfanya akatishe masomo ya sekondari na kuanza kwenda kanisani kila wakati kwa ajili ya maombi.

MAUZAUZA KILA MARA
Chanzo kilisema kuwa, kipindi chote hicho, Neema alikuwa akianguka na kutaja majina ya watu wa  mtaani anapoishi kwamba ni wachawi, wengine wanahusika kumchukua yeye usiku na kwenda naye makaburini ambako humlisha nyama na kumnywesha damu za watu.
“Neema alikuwa akisumbuliwa na mapepo tangu akiwa mdogo na alikuwa anasumbua kwelikweli. Alipokuwa  akipandisha ‘madudu’ yake hayo hakuna aliyeweza kumshika labda wanaume kama watano. Pia kuna wakati alikuwa akitaka kujiua kwa kujichoma kisu,” kilisema chanzo hicho.
Mama mzazi wa Neema.
MAMA MZAZI ASIMULIA
Naye mama mzazi wa Neema ambaye hakupenda kujitambulisha kwa jina,  alipozungumza na gazeti hili huku majirani wakifurika nyumbani kwake, alisimulia jinsi mwanaye huyo alivyokuwa akiteseka kipindi chote tangu alipokuwa mdogo mpaka ikafika hatua amepata ujauzito huo na hatimaye kujifungua kiumbe kinachofanana na chatu.
“Ni mambo mengi ambayo tumeyapitia lakini siwezi kumkufuru Mwenyezi Mungu kwa sababu mpaka leo hii tuko wazima japo mitihani ni kipimo cha maisha na hata hili lililotokea karibuni ni mtihani pia, ila kikubwa ni kuomba sana.
“Baada ya kupata huu ujauzito kuna wakati tulikuwa hatulali, akianza kulia ni  usiku kucha, anasema kuna kitu kinambana kifuani. Tulipokuwa tukienda hospitali kwa ajili ya uchunguzi, vipimo vilionesha mtoto tumboni hachezi.
“Mimi kama mzazi, hayo mambo yaliyokuwa yanamtokea mwanangu nilikuwa nayaona kama maajabu f’lani hivi japokuwa kipindi hicho alikuwa mzima na mimi mwenyewe nilikuwa nikimsubiri mjukuu  wangu kwa hamu, kumbe tunakuja kupokea kitu cha ajabu namna ile,” alisema mama huyo.
SIKU YA KUUMWA UCHUNGU
Iliendelea kudaiwa kuwa, kipindi chote cha ujauzito, Neema alikuwa mtu wa maombi, lakini siku ya kuumwa uchungu alikimbizwa hospitali (haikutajwa jina) na kujifungua kiumbe cha ajabu. Ndipo familia ikaamua kukaa kikao na kuamua kukizika  kiumbe hicho kama chatu.
Mama Neema anasema: “Mwanangu alijifungua kiumbe cha ajabu, kilikuwa kama chatu halafu kina magamba na  meno mawili marefu lakini hakikuwa hai. Tulishtuka sana, tukaona ni mkosi katika familia lakini tuliamua kukizika kile kiumbe.“Sikuona sababu ya kuwaonesha majirani zangu kwa kuwa kilikuwa kinatisha. Ila naona ni bora niwape taarifa kuwa, mwanangu alijifungua kiumbe cha ajabu.”
ALICHOSEMA ALIYEJIFUNGUA
Naye Neema mwenyewe alipozungumza na Amani kuhusu tukio hilo la ajabu, alikuwa na haya ya kusema:“Mimi mwenyewe sikupenda kuzaa chatu jamani, nimepitia mambo mengi ya ajabu, wazazi wangu ndiyo wanajua fika hali niliyokuwanayo huko nyuma, lakini sina namna.
“Labda niwaulize mama zangu ambao tayari walishazaa kama tumbo huwa linapanda juu mpaka kifuani badala ya kushuka? Na nilikuwa nakabwa sana kuanzia kifuani mpaka kwenye koo, usiku sikuwa nalala kutokana na maumivu niliyokuwa nikiyapata mpaka nilipojifungua hicho kiumbe.
“Usione watu tunatembea, hatujijui tuna nini kwenye miili yetu. Leo hii yamenikuta mimi, kesho mtu mwingine. (huku akiwaangalia majirani) mi nawaomba ndugu zangu tukazane kumwomba Mungu kwani mimi maombi yamenisaidia sana.”

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate