EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, April 15, 2015

MASOGANGE ATIMULIWA SAUZ!

Sifael Paul na Imelda Mtema
HABARI ikufikie kuwa muuza nyago wa video za wasanii wa Bongo Fleva (video queen), Agness Gerald ‘Masogange’ anadaiwa kutimuliwa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ na sasa amekuwa akionekana Bongo akirandaranda mitaani.
Muuza nyago wa video za wasanii wa Bongo Fleva (video queen), Agness Gerald ‘Masogange’.
TUJIUNGE JOHANNESBURG
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho Masogange ni rafiki yake aliyeko maeneo ya Midland jijini Johannesburg, Sauzi, staa huyo alitimuliwa na mwenye nyumba baada ya kodi ya pango kwisha na kutakiwa kulipa jambo ambalo lilimshinda.
Ilisemekana kwamba mwanaume aliyekuwa akimpa jeuri aliyetajwa kwa jina maarufu la Said 2010 ambaye ni mfanyabiashara, Mbongo aishie jijini humo alimtosa hivyo bidada akarejea Bongo kinyemela.
KUMBE CHANZO NI TUNDA
Habari nzito zilidai kwamba chanzo cha jamaa huyo ‘kumfungia vioo’ Masogange ni baada ya kunasa kwenye penzi la muuza nyago mwingine wa video za wasanii wa Kibongo aliyetajwa kwa jina maarufu la Tunda.
Ilidaiwa kwamba zile mbwembwe za Masogange za kujitundika mitandaoni zilifika mwisho baada ya Said kuhamia kwa Tunda, mtoto mweupe mwenye sura ya mvuto ambaye anaonekana kwenye video za nyimbo za akina Matonya, TID ‘Mnyama’, Christian Bella na wengine wengi.Ilizidi kunyetishwa kwamba, awali, Tunda alikuwa Bongo lakini jamaa huyo alimtumia tiketi ya ndege na sasa anatanua naye Bondeni kwa Madiba.
Masogange akipozi.
UGOMVI
Ubuyu uliendelea kumwagwa kwamba, hivi karibuni Masogange na Tunda waliingia kwenye ugomvi mkubwa huku wakitukanana mitandaoni bila kuanika sababu ya bifu lao.
“Kama ulikuwa unamfuatilia Masogange wiki mbili hivi zilizopita, utagundua kuna mtu alikuwa anagombana naye. Si mwingine ni huyo Tunda ambaye amemdatisha jamaa hadi akasahau kama kuna Masogange.

“Wewe fikiria, Masogange siyo mtu wa kutua Bongo kimyakimya bila kutupia picha kwenye Instagram ili kuwarusha roho wenzake. Siyo kwamba hawezi, sasa hivi yupo juu ya mawe ndiyo maana anajificha,” kilisema chanzo hicho.
SUALA LA URAIA
Chanzo hicho kilipotonywa kuwa mwaka jana Masogange alitamba kuukwaa uraia wa Sauzi na kuukana wa Bongo kilisema:“Mimi nimeishi hapa South Africa (Sauzi) zaidi ya miaka mitano. Nilishaomba uraia miaka kibao sijapata hadi leo, huyo Masogange ni nani wampe uraia kwa siku mbili? Hizo fiksi tu. Kama aliomba sawa lakini hawezi kupewa uraia kirahisirahisi. Kuna process (taratibu) ndefu hadi mtu apate uraia.”
Pasport ya Agness Masogange.
MASOGANGE ATAKWENDA TENA SAUZI?
Chanzo hicho kilizidi kudadavua kuwa siyo kwamba Masogange hatakwenda tena Sauzi kwa sababu ana watu na marafiki kibao nchini humo lakini kwa sasa hana maskani ya kufikia baada ya kutimuliwa.“Anaweza kwenda any time (muda wowote) lakini mpaka awe na uhakika na pa kufikia,” kiliongeza chanzo hicho.
Baada ya kujazwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Masogange, alipopatikana alisomewa kila kitu ‘eituzedi’ ambapo aliomba chondechonde isiandikwe kwamba ametimuliwa bali yupo Bongo kwa ajili ya mapumziko.
“Jamani si kweli, waambie wahariri nipo huku (Bongo) kwa ajili ya mapumziko tu,” alisema Masogange kwa kifupi.
TUJIKUMBUSHE
Mwaka juzi Masogange alikamatwa Sauzi kwa msala wa madawa ya kulevya ambapo alihukumiwa kisha akalipa faini na kurejea Bongo kabla ya baadaye kutangaza kupata uraia nchini humo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate