MNENGUAJI tishio wa bendi ya FM Academia, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’, ameweka wazi kwamba hakuchukizwa na ndoa ya siri ya aliyewahi kuwa mpenzi wake, Kalala Hamza ‘Kalala Jr.’ kwa kuwa walishaachana.
Queen Suzy alisema waliachana na mwanamuziki huyo anayeitumikia bendi ya Twanga Pepeta miaka nane iliyopita, hivyo hana wivu tena na mwanamume huyo na sasa anampongeza kwa kuwa alitumia muda mwingi kumtafuta mwanamke wa kumuoa.
“Si kweli kwamba nimechukia kuoa kwa Kalala kwa kuwa tulishaachana na Kalala takribani miaka nane na sijawahi kurudiana naye, hivyo sina wivu naye, nimefurahi na nampongeza kwa kuoa, tena namuombea aishi kwa amani na furaha katika ndoa yake,” alisema Queen Suzy.
Queen Suzy aliongeza kwamba kutokana na kutumia muda mwingi kupata mwanamke wa kuoa, Kalala anastahili pongezi na sala nyingi ili maisha yake ya ndoa yadumu muda mrefu.
Kalala Jr. mwishoni mwa wiki hii alimuoa aliyekuwa mchumba wake wa siku nyingi, Muna Alphone, katika harusi ya kimya kimya.
CHANZO: MTANZANIA
No comments:
Post a Comment