EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, April 17, 2015

SIRI YA MAPENZI YAO IKO MOYONI MWAO

Mwandishi Wetu
Mastaa wengi wamekuwa wakiingia kwenye uhusiano na kufanya siri kubwa. Wapo ambao wanaonekana dhahiri ni wapenzi kutokana na ukaribu wao lakini wakiulizwa wanadai wana ‘project’.Ukiuliza ni project gani utaambiwa wana filamu wanacheza. Cha ajabu sasa unaweza kusubiria hiyo filamu na usiione. Mwisho wa siku unajiongeza na kubaini baadhi wanatumia kivuli cha ‘project’ kuendesha penzi lao kwa siri.
Juma Musa ‘Jux’ na Vanessa Mdee.
Utakumbuka hata uhusiano wa mwanamuziki Nasibu Abdul “Diamond’ na Zarina Hassan ‘Zari’ walianza kwa staili hii. Walijifanya wana kazi ya kisanii wanafanya lakini kumbe wameshazimikiana na mpaka leo hii ni wapenzi wanaotarajia kupata mtoto.
Katika siku za hivi karibuni hapa Bongo kuna wasanii ambao nyendo zao zinaonesha wazi ni wapenzi lakini wenyewe wamekuwa wagumu kuweka wazi. Ifuatayo ni orodha ya mastaa hao ambao ni kama wako penzini lakini ushahidi wa wazi hamna.

Juma Musa ‘Jux’ na Vanessa Mdee
Wanamuziki hawa wamekuwa wakiongozana kila kona, wakati mwingine wakitupia picha za kimahaba huku watu wao wa karibu wakieleza kuwa ni wapenzi.Hata hivyo, hakuna hata mmoja kati yao aliyewahi kukiri kwamba wanatoka hivyo suala la kwamba ni wapenzi au siyo linabaki kuwa siri yao.
Shamsa Ford na Nay wa Mitego.
Shamsa Ford na Nay wa Mitego
Hawa ni mastaa ambao ni gumzo mjini. Uhusiano wao kiasi cha kupiga picha wakidendeka na kuzitupia mtandaoni na hata Shamsa kulala nyumbani kwa Nay kumewafanya wengi waamini ni wapenzi.
Majibu yao wanapoulizwa wanadai eti wako kwenye project ya filamu. Mimi na wewe hatuwezi kujua ukweli lakini mwenye macho haambiwi tazama. Yaani hata kama ni filamu lakini kuna kitu zaidi ya filamu.
Aunt Ezekiel na Moze Iyobo.
Aunt Ezekiel na Moze Iyobo     
Kila mmoja ukimuuliza mimba ya Aunt ni ya nani atakuambia ni ya Moze lakini baadhi bado haiwaingii akilini.
Wapo wanaohisi Moze ni boya tu bali kuna mhusika wa mimba hiyo ambaye huenda hataki kujulikana.
Kilichoibua utata zaidi ni kitendo cha hivi karibuni cha Moze kumuita Aunt dada, watu wakabaki..haah! Dada tena!
Ni kweli haishindikani Aunt kuamua kuzaa na kijana huyo lakini majibu ya Moze wakati mwingine yamekuwa yakiwafanya watu wahisi kuna ‘kafilamu’ kanachezwa. Yetu macho, sijui akizaliwa mtoto Mwarabu wakati Moze ni mweusi itakuwaje.
Husna Sajent na Salim Ahmed ‘Gabo’
Madai kuwa wasanii hawa ni wapenzi yamekuwa yakishika kasi kila siku hadi ikafikia hatua ikadaiwa wamefunga ndoa ya siri na picha zao zikavuja.Kama ilivyo kawaida, wasanii hao kwa nyakati tofauti wakadai eti picha zilizovuja zikionesha wamefunga ndoa ni filamu. Tumebaki njia panda tusijue ukweli ni upi. Huenda mioyoni mwao wanajua ni wapenzi lakini wanafanya siri kwa sababu wanazojua wenyewe.
Muna na Kalala
Rose Alfonce  a.k.a Muna au Pacha wa Mainda anadaiwa kuwa kwenye uhusiano uliokolea na Mwanamuziki Kalala Junior. Wafuatiliaji wa mambo wanadai kuwa, penzi lao limekuwa ni kama mke na mume kwani wakati mwingine Kalala hulala nyumbani kwa Muna maeneo ya Mwananyamala.
Wenyewe wakiulizwa wanachengachenga, hasa Muna lakini kwa watu wenye akili zao wanaona kabisa ni wapenzi kiasi kwamba siku tukisikia wamefunga ndoa hatutashangaa.
Kuonesha kwamba hawa watu ni wapenzi, Kalala juzikati alianika hisia zake kwa kutunga wimbo ulioelezwa kuwa ni maalumu kwa mpenzi wake huyo.
 

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate