Ofisa wa sanaa kutoka Balaza la sanaa (BASATA)Augustino Kihiyo(kushoto) John Saimon 'Joh Makin'(katikati) pamoja na G-Nako.
Baadhi ya wasanii na wanafunzi wa Chuo Cha Habari cha DSJ wakifuatilia mkutano huo.STAA wa muziki wa Hip Hop Bongo, ambaye pia ni memba wa Kundi la Weusi kutoka Arusha, John Simon ‘Joh Makini leo amefungukia wasanii wenzake kukubali kukosolewa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila baada ya wiki mbili katika Ukumbi wa Basata-Sharif Shamba, Ilala jijini Dar es Salaam, Joh amesema kuwa ili kuweza kupambana changamoto za muziki katika jamii ni lazima kukubali kukosolewa.
“Tunatakiwaa kutengeneza muziki unaokubalika katika soko kwani msanii anayetaka kutoka kimuziki lazima ajitambue katika jamii yake,” alisema Joh Makini anayetamba kwa sasa na Wimbo wa Nusunusu.
(PICHA/HABARI: DENIS MTIM/GPL)
No comments:
Post a Comment