Ijumaa: Vipi kuhusu sakata lako la nguo kukuvuka ukiwa jukwaani limekuathiri kivipi?
Shilole: Halijaniathiri chochote hiyo ni kama mtu anapata ajali akiwa kazini.
Ijumaa: Wakati zile picha zilipokuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii, mpenzi wako Nuhu alilizungumziaje hilo?

Shilole: Hakuzungumza chochote kwani tulikuwa pamoja siku ya tukio hivyo anajua nini kilitokea.
Ijumaa: Najua una wakwe, je, walipoziona hizo picha hawakumsumbua Nuhu na kuona kama unawadhalilisha?
Shilole: Hapana, tena walikuwa upande wangu sana na kuniambia nisijali.
Ijumaa: Nini ulichojifunza kupitia tukio hilo?
Shilole: Nimejifunza vitu vingi sana, siwezi kufanya shoo bila kupima nguo yangu vizuri.
Ijumaa: Vipi kuhusu ishu ya kumpiga mwanamke aliyedai ana mimba ya Nuhu?
Shilole: Hiyo ishu siyo ya kweli hata kidogo kwa sababu alikiri kuwa alitumwa ili aharibu mapenzi yetu.
Ijumaa: Vipi kuhusu tamko la Basata kutokana na nguo kukuvuka jukwaani?
Shilole: Hamna shida, kwa sasa nimeshamalizana nao.
Ijumaa: Suala lako la nguo kukuvuka lilizungumziwa mpaka bungeni, vipi ulijisikiaje viongozi wa nchi kukujadili kwa suala kama hilo?
Shilole: Kwanza nilifarijika sana na kuona hata viongozi wanafuatilia kazi zangu na wanatambua mchango wangu ndiyo maana waliweza kuongelea ishu hiyo.
Ijumaa: Mumevalispete ya uchumba kitambo sasa, vipi kuhusu ndoa? Maana uchumba hautakiwi kuwa wa muda mrefu.
Shilole: Ndoa inakuja soon, zimebaki siku chache sana tunaweka mambo sawa utaishuhudia tu.
Ijumaa: Wewe tayari una watoto wawili, vipi Nuhu analichukuliaje hilo?
Shilole: Hana neno kwa kuwa ananijua historia yangu kabla hatujawa wapenzi na anawapenda sana watoto wangu.
Ijumaa: Vipi kuhusu kuzaa na Nuhu?
Shilole: Yaani mimba ikiingia ni sawa kwa sababu hatutumii
No comments:
Post a Comment