Utumishi! Mwigizaji mkongwe Bongo, Julieth Samson Kakuru ‘Kemmy’ aliyewahi kutamba kwenye Tamthiliya za Kundi la Kaole Sanaa na filamu ya Nguvu ya Imani, ameibukia kwenye huduma ya Uinjilisti kupitia kanisa analoabudu la Miaron ya Mamle lililopo Mbezi Kwamsuguri jijini Dar.Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Kemmy alifunguka:
“Mbali na filamu, kwa sasa natoa huduma ya Uinjilisti kwa kuzunguka katika makanisa mbalimbali, nimewahi kutoa huduma kwa wanawake wenye matatizo ya watoto na Mungu akatenda, sasa wana watoto.”
Msanii huyo aliongeza kuwa, ameamua kufanya kazi hiyo kwa sababu kumtumikia Mungu ni jambo jema na la baraka tofauti na kuwa bize na mambo ya dunia ambayo hayana faida yoyote.
No comments:
Post a Comment