EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, June 18, 2012

NIPASHE :Kituo cha mabasi Mwenge chakithiri kwa rushwa

  Mabaunsa waunda umoja
Watu wanaodaiwa kuwa ni "mabaunsa" wameunda umoja wao na kuanza kukusanya ushuru kutoka kwa Wamachinga wanaopanga bidhaa zao katika kituo cha daladala cha Mwenge Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mabaunsa hao wamedaiwa kufanya zoezi hilo huku wakishirikiana na baadhi ya watendaji wa Manispaa ya Kinondoni ambao wanawapa sehemu ya mapato wanayoyapata kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE umebaini kuwa "mabaunsa" hao ni sehemu ya wafanyakazi wa iliyokuwa kampuni iliyopewa tenda ya kukusanya ushuru wa daladala katika kituo hicho ambayo hata hivyo inadaiwa imemaliza muda wake wa kufanya kazi hiyo.
Watu hao wanadaiwa kukusanya kati ya Sh. 500,000 hadi 1,000,000 kutegemea wingi wa wafanyabishara kwa siku hiyo ambao wanapanga bidhaa zao kwenye meza na wengine wanaozishika mikononi kuanzia asubuhi hadi usiku.

Baadhi ya wafanyabishara hao ambao wanaendesha bishara zao kituoni hapo, waliliambia NIPASHE kuwa meza moja inalipiwa kati ya Sh. 5,000 hadi Sh. 7,000 kutegemea na ukubwa wa meza na kwamba fedha hizo zinatolewa kila siku.
Katika kituo hicho kuna zaidi ya meza 100 zilizozunguka eneo zima huku idadi ya wamachinga wanaotozwa ushuru bila ya kuwa na meza ikiwa haijulikani lakini fedha hizo zinadaiwa kuchukuliwa na mabaunsa bila kutoa stakabadhi.

Wamesema mtu anayekataa kulipa ushuru huo, anapigwa na watu ambao walidai wana miili mikubwa pamoja na kuwanyang'anya bidhaa zao zilizopo mezani na kwa wale wanaokuwa wamezishika mikononi.
Hata hivyo, walisema licha ya kulipa kiasi hicho cha fedha hawapewi stakabadhi na kwamba mfanyabiashara anayejaribu kudai anapigwa na kupelekwa kituo kidogo cha Polisi Mwenge.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwenge, Pascal Ng'itu alikiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema kuwa watu hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi sasa.

Alisema wafanyabiashara hao licha ya kuwa wapo katika eneo hilo kinyume cha sheria lakini kimeibuka kikundi cha watu wanaowalipisha ushuru huku mapato hayo yakiwa hayajulikani yanapelekwa wapi.
Alifafanua kuwa kwa muda wa mwaka mmoja, hakuna Mkandarasi anayejulikana kisheria ambaye amepewa kazi ya kukusanya mapato yatokanayo na ushuru wa magari ya daladala yanayotumia kituo hicho.
Ng'itu alisema kwamba kampuni iliyoshinda tenda ya kukusanya mapato katika kituo hicho, imenyimwa kazi hiyo na badala yake watu wasiojulikana ndiyo wanaoendelea kukusanya fedha zinazolipwa na daladala.

"Hiki kituo mimi kama mwenyekiti naona kuna uchafu mwingi na wa kutisha kwa sababu watu wanaokusanya ushuru haijulikani wanazipeleka wapi na ni kiasi gani kinachopatikana," alisema
Kwa mujibu wa taratibu za Manispaa ya Kinondoni, kampuni inayopewa tenda ya kukusanya ushuru inatakiwa kusimamia mapato yatokanayo na daladala, kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo, kukiweka kituo katika hali ya usafi pamoja na kuwaondoa wapiga debe.
Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Kinondoni, Fortunatus Fwema alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema ameshtushwa huku akisema kwamba hajui kama kuna kikundi cha watu kinakusanya ushuru kutoka kwa wamachinga.

Alisema wamachinga hao wapo kituoni hapo kinyume cha utaratibu, lakini akasema pia watu wanawatoza ushuru wanahesabiwa kama wahalifu na kwamba watasakwa na Manispaa.
Alisema juhudi za kuwaondoa wamachinga pamoja na kumpata mkandarasi wa kukusanya ushuru zinafanyika na kwamba siku yoyote kuanzia sasa watavamia kituo hicho ili kuwatoa.
Alisema baada ya kumaliza kazi ya kuwaondoa wamachinga katika eneo la Ubungo na Tegeta kwa sasa zoezi hilo litahamia Mwenge muda wowote ili kuhakikisha kituo kinabaki wazi kwa ajili ya kuhudumia daladala.
Aliahidi kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini watendaji wa Manispaa wanaoshirikiana na kikundi hicho kukusanya ushuru kinyume cha sheria wala kufuata taratibu.
                                   CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate