
Kaka mkubwa wa marehemu aliyekuwa
Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde, George Ongiri
Ogunde (wa kwanza kulia) akishirikiana na ndugu, jamaa na waandishi wa
habari, kubeba mwili wa mhariri huyo, aliyefariki dunia ghafla jana
usiku eneo la Forest Hill, mjini Morogoro. Mwili huo ulikuwa unatolewa
chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa
ajili ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya
mazishi katika Kijiji cha Mugumu kilichopo wilaya ya Serengeti, mkoani,
Mara..

Mbunge wa Jimbo la Morogoro, Azizi
Abood, akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006),
Husein Bashe wakisubiri kuuona mwili wa Willy Edward

Baadhi ya waandishi wa habari
akiwemo Mbunge wa Morogoro mjini, Azizi Abood, wakiwa na huzuni
walipokuwa wakisubiri kutoa heshima za mwisho katika Hospitali ya Rufaa
ya Morogoro, muda mfiupi kabla ya mwili kusafishwa Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel
Bendera (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa kaka mkubwa wa marehemu
aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde,
George Ongiri Ogunde muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda jijini
Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika kijiji cha cha Mgumo
kilichopo wilaya ya Serengeti mkoani Musoma. wa pili kutoka kulia ni
Katibu Tawala wilaya ya Morogoro, Alfred Shao na kaka mkubwa upande wa
baba, Isack Ugunde.
No comments:
Post a Comment