Waziri wa zamani wa Misri Sahem Fahmi
amehukumiwa kifungo cha miaka kumi na tano gerezani kutokana
na kuiuzia Israel gesi asili kwa bei ya chini sana.
Bwana Fahmi amepatikana na hatia ya ubadhirifu wa mali ya umma.
Mfanya-biashara aliyehusishwa kwenye
kashfa hiyo Hussein Salem naye amepewa kifungo kama hicho, akiwa
mwenyewe hayuko Mahakamani.
Waendesha mashitaka wamesema mauzo ya
gesi kwa bei nafuu kwa nchi ya Isreal yaliofanywa na serikali ya zamani
ya Hosni Mubarak kumeigharimu serikali faida ya mamilioni ya dola.
No comments:
Post a Comment