SIKU chache baada ya SSRA inayosimamia mifuko ya pensheni hapa nchini
kutoa waraka wa kuzitaka Taasisi pamoja na Makampuni ikiwemo migodi ya
madini kutowalipa mafao yao wanapoacha kazi, mpaka wafikishe umri wa
miaka 55, baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya African Barrick Gold Mines
Ltd wamejitokeza kuaacha kazi wakipinga hali hiyo.
Wafanyakazi hao kutoka migodi ya Dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi iliyopo wilayani Kahama ambayo inamilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold Mines Ltd ambao wengi wao ni wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii [ NSSF]wameaandika barua za kuacha kazi kwa madai uamuzi huo umeamuliwa bila kuwashirikisha.
Pamoja na SSRA kusambaza waraka kwenye mifuko hiyo kote nchini ikieleza ratiba ya kupita ikitoa elimu kwa wanachama wa mifuko hiyo juu ya mabadiriko yaliyojitokeza kwa lengo la kuboresha zaidi lakini wafanyakazi hao wengi wao wamepinga vikali wakidai hali hiyo ina lengo la kudhurumu fedha zao ambazo huzichangia kila mwezi kutoka kwenye mishahara yao.
Walidai uamuzi huo wa kuchukua mafao yao baaada ya kufikisha umri wa miaka 55 hauko sawa kutokana na wengi wao kutokuwa na ajira za kudumu kwenye makampuni ambayo hufanya kaza kwa mikataba ya miaka michache na yanapomaliza kufanya kazi huondoka nchini na wao kukosa kazi,hivyo kusubiri muda wa umri wa miaka 55 ndipo walipwe mafao yao hapo hakuna haki.
Frederick Katulanda
via google.com/MabadilikoTanzania

No comments:
Post a Comment