Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dkt. Steven Ulimboka amewasili Afrika ya Kusini kuanza kupatiwa matibabu.
Dkt. Ulimboka alisafirishwa juzi kwa ndege ya kukodi ya Shirika la Ndege la Afrika ya Kusini kwenda nchini humo, baada ya hali yake kubadilika ghafla Alhamisi wiki iliyopita.
Jopo la Madaktari lililokuwa likimhudumia Dkt. Ulimboka lilitoa taarifa kuwa figo zake zimeshindwa kufanya kazi na juhudi zao kusafisha damu yake kutokutoa matokeo mazuri, hivyo kushauri apelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi.
Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dkt. Edwin Chitage alilieleza gazeti la MWANANCHI kuwa, Dkt. Ulimboka alifika salama Afrika ya Kusini na kuwa kwa sasa anaendelea na matibabu, “Habari nilizopata kutoka Afrika Kusini zinaeleza kuwa amefika salama jana (juzi) na anaendelea vizuri baada ya kupata huduma zinazohitajika,”alisema.
Dkt. Chitage ambaye hakuwa tayari kutaja ni hospitali gani anatibiwa, alisisitiza kuwa huduma alizozipata nchini humo zimenza kumsaidia.
Hata hivyo, habari zaidi zilizopatikana jana zilieleza kuwa Dkt. Ulimboka wenzake wawamekataa kata kata kutaja hospitali hiyo kwa sababu za kiusalama, na kwamba hali yake ilikuwa bado haijabadilika sana, “Hakuna mabadiliko yoyote, walifika salama jana (juzi) na kwa kuwa anatibiwa katika hospitali ya kulipia, huduma zimeanza jana (juzi) ileile,” alisema daktari mmoja ambaye yupo karibu na Dkt. Ulimboka.
Ulimboka.Via Mwananchi

No comments:
Post a Comment