Shirikisho la soka la bara la ulaya UEFA limemtangaza kiungo wa Spain Andres Iniesta kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Euro 2012.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 alianza kwenye mechi zote sita za Euro na akucheza kama kiungo mshambuliaji na kuiwezesha timu yake ya La Roja kubeba ndoo jana usiku.

Iniesta ambaye alichaguliwa na watu 11 wa jopo la ufundi la UEFA, alitoa assist moja katika dakika dakika 551 alizocheza kwenye Euro 2012.

Pia yupo kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa UEFA wa michuano hiyo, ambacho pia kimebeba wachezaji 10 wa Spain na wanne wa Italy.

Cha kushangaza zaidi mfungaji bora wa mashindano Fernando Torres hayupo kwenye kikosi, kucheza dakika 189 kukionekana kuwa sababu kubwa, Mario Balotelli, Cesc Fabregas, Cristiano Ronaldo, Zlatan Ibrahimovic na David Silva ndio wanaounda safu ya ushambuliaji.

HIKI NDIO KIKOSI CHA MICHUANO HIYO KILICHOCHAGULIWA NA UEFA
Goalkeepers:
Gianluigi Buffon (Italy), Iker Casillas (Spain), Manuel Neuer (Germany)
Defenders: Gerard Pique (Spain), Fabio Coentrao (Portugal), Philipp Lahm (Germany), Pepe (Portugal), Sergio Ramos (Spain), Jordi Alba (Spain)
Midfielders: Daniele De Rossi (Italy), Steven Gerrard (England), Xavi (Spain), Andres Iniesta (Spain), Sami Khedira (Germany), Sergio Busquets (Spain), Mesut Ozil (Germany), Andrea Pirlo (Italy), Xabi Alonso (Spain)
Attackers: Mario Balotelli (Italy), Cesc Fabregas (Spain), Cristiano Ronaldo (Portugal), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), David Silva (Spain).