EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, July 25, 2012

Hosptali ya AICC kuendesha kampeni ya kupima kisukari bure

digg Wachezaji wa Azam wakishangilia bao la pili lililofungwa na mshambuliaji John Boko katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Azam ilishinda 3-1. Picha na Michael Matemanga. Sosthenes Nyoni MSITU wa Pande ni jina maarufu nchini kwa sasa kutokana na matukio ya watu kutekwa na kupelekwa huko kuteswa na  kuuwawa kinyama. Kitendo kama hicho cha kinyama ndicho kinachofananishwa na ilichofanyiwa Simba  jana na mshambuliaji wa Azam, John Boko baada ya kufunga mabao matatu pekee na kuiwezesha timu yake kushinda 3-1 katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.  Kwa ushindi huo sasa Azam itacheza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya AS Vita ya DR Congo iliyoitoa Atletico ya Burundi kwa mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa awali. Boko alifunga bao lake la kwanza dakika 17, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Ibrahimu Shikanda, kisha akapachika la pili kwa shuti dakika 46 akimalizia pasi ya Kipre Tchetche, kabla ya Shomari Kapombe kuifuta machozi Simba dakika 53, lakini Boko mfungaji bora wa msimu uliopita alizima ndoto za Simba kurudi kwa kupachika bao la tatu kwa shuti la chini lililomshinda Juma Kaseja na kujaa wavuni.   Katika kile kinachoonekana kujaa kwa imani za kishirikina jana klabu za Simba na Azam hazikutumia mlango mkuu wa kuingilia uwanjani baada ya kumaliza kufanya mazoezi. Simba wenyewe walitokea geti la kaskazini na Azam walipita mlango tofauti wakati wakirejea vyumbani tayari kujiandaa na mechi hiyo. Simba ilianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kufika  langoni kwa Azam katika dakika ya kwanza na saba, lakini Haruna Moshi na Felix Sunzu na Uhuru Selemani walishindwa kutumia nafasi hizo. Katika mechi hiyo Sunzu alipewa kadi ya njano na mwamuzi Issa Kangabo kutoka Rwanda kwa kumchezea vibaya Tchechte. Mwanzoni mwa kipindi cha kwanza Uhuru Selemani alipoteza nafasi mbili za kufunga baada ya kuwatoka mabeki wa Azam, lakini jitihada zake ziliishia mikononi mwa kipa Deogratius Munishi, huku Azam wakijibu mapigo dakika 14 baada ya Kipre kuwatoka mabeki wa Simba na kupitisha pasi kwa Hamis Mcha aliyepiga fyongo shuti lake. Dakika ya 17 beki Shikanda wa Azam alipokea pasi ndefu kutoka katikati ya uwanja na kupiga krosi iliyotua kichwani kwa Bocco ambaye alipiga kichwa kilichokwenda wavuni na kumwacha Kaseja akiwa amesimama. Simba walijaribu kurudi mchezoni, lakini mashuti ya Kapombe na Mwinyi Kazimoto dakika 34 na 36 yalishindwa kulenga goli. Dakika 41 mwamuzi aliinyima Simba penalti baada ya Kazimoto kumuangusha Ramadhan Chombo kwenye eneo la hatari. Azam  walianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika 46 kupitia Boko aliyemalizia vizuri kazi ya Tchetche aliyekuwa mwiba kwa ngome ya Simba. Mchezaji bora wa mwaka wa Taswa, Kapombe aliifungia Simba bao dakika 53 akipokea krosi ya Haruna Shamte na kupiga shuti kali akiwa ndani ya 18 lililomshinda Munishi. Kocha wa Azam, Stewart Hall aliwapumzisha Tchetche, Mcha na kuwaingiza George Odhiambo na Jabir Aziz, wakati Simba ilimtoa Uhuru, Jonas Mkude, Mudde Musa na kuwaingiza Kigi Makasi, Amri Kiemba na Hamis Kinje. Mabadiliko hayo yalionekana kuwa na faida kwa Azam kwani dakika 73, Aziz alitoa pasi kwa Boko na kupiga shuti la chini akiwa nje ya 18 na kwenda moja kwa moja wavuni na kuwanyamazisha kabisa mashabiki wa Simba.   Awali Atletico ya Burundi inayosifiwa kwa kucheza soka ya kuvutia iliyaaga mashindano hayo kwa kuchapwa mabao 2-1 na AS Vita ya DR Congo. Mshambuliaji Etekiama Taddy alifunga bao lake la sita kwenye michuano hiyo alipozifumania nyavu za Atletico katika dakika ya 8 na kuifanya AS Vita kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa bao 1-0. Atletico ilirudi vizuri na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika 48 kwa shuti kali lililopigwa naPierre Kwizera akiitumia vizuri pasi iliyopigwa na Henry Mbazumutima. Wakati mashabiki wakidhani mpira huo utaamuliwa kwa mikwaju ya penalti, mshambuliaji Basilua Makola aliifungia AS Vita bao la ushindi katika dakika za nyongeza na kufanya mchezo huo kumalizika kwa 2-1. Nusu fainali ya michuano hiyo itaendelea tena kesho kwa Azam kuivaa AS Vita saa nane mchana na mabingwa watetezi Yanga kupepetana na APR saa kumi jioni kwenye Uwanja wa Taifa. By Mwananchi
Arusha, Tanzania.
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha kupitia hospitali yake ya AICC kitaendesha kampeni ya kupima kisukari bure kwa wakazi wa Arusha ili kusaidia wananchi kutambua kama wana ugonjwa wa kisukari au wapo katika hatari ya kuugua ugonjwa huo.

Kampeni hiyo itafanyika kesho (terehe 26-07-2012) katika hopitali ya AICC iliyopo jijini Arusha ambapo madaktari wa hospitali ya AICC kwa kushirikiana na madaktari wa wanaohudhuria mkutano wa Shirikisho la Madaktari wa Kimataifa pamoja na madaktari kutoka Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania wataendesha zoezi la upimaji huo.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, Bwana Elishilia Kaaya, amesema kuwa mbali na kupima kisukari, madaktari hao pia watatoa ushauri wa namna bora ya kuishi na jinsi ya kuzuia madhara ya kisukari kwa wale watakao kuwa wamekutwa na ugonjwa huo.

 “Hospitali ya AICC inatambua umuhimu wa afya za wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla na ndio maana tumeona ni vema kufanya kampeni hii ya kupima kisukari. Napenda kutumia fursa hii kuwaalika wakazi wote wa Arusha na vitongoji nyake kufika kwa wingi kwani mbali na kupima pia itatolewa elimu na ushauri kutoka kwa wataalamu hao.” alieleza Kaaya.

Kwa mujibu Mkurugenzi Mwendeshaji, upimaji huo utaenda sambamba na mkutano wa kwanza wa Shirikisho la Madaktari wa Kisukari wa Kimataifa ambao kwa mara ya kwanza unafanyika hapa nchini. Mkutano huo utafanyika katika kituo cha AICC ambapo madaktari wanaohudhuria mkutano huo na wale kutoka Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania watatoa huduma ya upimaji katika zoezi hilo.

“Tunaamini baada ya kampeni hii wananchi watakuwa wamepata ufahamu juu ya hali ya afya zao na kutumia vema ushauri wa madaktari kwa ajili ya kujikinga na kuzua athari za ugonjwa huo”, alielezea Kaaya.

Mbali na kuendesha kampeni hii, hospitali ya AICC imeanzisha kitengo maalumu cha kisukari ambapo kila wiki madaktari hutoa huduma za matibabu na ushauri kwa wagonjwa wa kisukri.

Ugonjwa wa kisukari umekuwa ukiongezeka kwa kasi duniani ambapo taarifa za Shirika la Afrya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 2011 watu milioni 366 walikuwa wanaugua ugonjwa wa kisukari na mwaka 2030 idadi inakadiriwa kufika milioni 552. Barani Afrika watu milioni 14 na nusu wanaugua ugonjwa huo huku idadi ikitarajiwa kufika milioni 28 mwaka 2030 ikiwa ni ongezeko la asilimia 90.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate