KOCHA wa APR ya Rwanda, Ernest Brandy amesema mchezo wao wa nusu fainali
dhidi ya Yanga utakuwa ni wa kulipiza kisasi tu si zaidi ya hapo.APR na
Yanga zitakutana kesho katika hatua ya nusu fainali ya kwanza
katika pambano litakalotegemewa kuwa na upinzani wa aina yake kutokana
na timu hizo kukutana kwenye hatua ya makundi na mabingwa watetezi
kushinda 2-0.
Akizungumza mara baada ya mchezo wa Yanga na Mafunzo kumalizika, kocha Brandy alisema mchezo wao utakuwa ni wa kulipiza kisasi si kingine.
Alisema wanakutana na Yanga kwa mara ya pili wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa awali hivyo wanaingia wakijihami zaidi na kuhakikisha wanashinda kwa kulipiza kisasi cha kufungwa magoli mawili hivyo wanahitaji zaidi ya magoli mawili.
"Ninakutana na Yanga, timu iliyotufunga mabao mawili katika hatua ya makundi, tutaingia uwanjani kwa kujihami zaidi huku tukitumia nafasi tutakazopata kuhakikisha tunashinda na kusonga mbele,"alisisitiza kocha huyo.
Aidha baadhi ya wachezaji wa APR wameonekana kutokuwa na hofu juu ya wapinzani wao na wamesisitiza nia yao ni kuingia hatua ya fainali na kuwavua ubingwa Yanga.
"Hata kabla Yanga haijacheza na Mafunzo nilikua na uhakika ndio timu tutakayokutana nayo katika nusu fainali, ni timu nzuri inayocheza kwa kujituma, lakini napenda kuwaambia walitufunga kwa bahati mbaya katika mchezo wa kwanza na kwa sasa tupo imara na wasitegemee ushindi,"alisema Kabange Twite.
Naye Seleman Ndikumana alisema wanakutana na mchezo uliojaa hisia za mashabiki hivyo watacheza kwa tahadhari kubwa ili wafanikiwe kuingia hatua ya fainali.

No comments:
Post a Comment