
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo, Abubakari Rakesh katika mkutano wa kumtambulisha mdhamini huyo Jijini Dar es Salaam jana.
Alisema kuwa udhamini huo utasaidia kutatua baadhi ya kero zilizokuwa zinawakabili.
“Huu ndio utakuwa ufumbuzi wa matatizo yetu kwani tumekuwa tukilalamika kwa muda mrefu kuwa soko letu linaonekana kama boma la kale licha ya jitihada za serikali kusaidia katika suala hili,” alisema Rakesh.
Rakesh alisema kuwa udhamini huo utasidia wafanyabiashara wadogowadogo kuwa karibu na wasambazaji wa bidhaa mbalimbali jambo ambalo hapo awali halikuwepo.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Kampuni ya EAR promosheni, Fredy Kimiti alisema kuwa lengo la kudhamini soko hilo ni kulitangaza kupitia Vyombo vya Habari jambo ambalo litasaidia kuwavuta wateja na hata wawekezaji.
Kimiti alisema wafanyabiashara watapata faida kupitia udhamini huo kwani licha kulitangaza soko vilevile watapeleka kampuni mbalimbali ziweze kufanya kazi kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa hapo.
“Tutahakikisha kuwa kila mfanyabiashara atakuwa na uwezo wa kuweka bango la bidhaa yake nje ya soko hili jambo ambalo litasaidia kuwavuta wateja katika kizimba chake,” alisema Kimiti.
Kwa mujibu wa Kimiti, wataanzisha maonyesho kwa kila mwaka katika soko hilo ambayo yatakuwa kila Mwezi Septemba ambayo yatachukua siku 20 na kujumuisha bidhaa mbalimbali na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali.
Alibainisha kuwa wameweka mikakati ya kuhakikisha wafanyabiashara wanabakia katika soko hilo na kuwataka wananchi kujitokeza na kuacha ile dhana ya kuwa machinga complex ni kwa ajili ya watu wa kipato cha chini.
No comments:
Post a Comment