Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati hiyo iliyosainiwa na Lyato, wameamua hivyo kutokana na mrufani, Ishabakaki Luta
kushindwa kutimiza matakwa ya kanuni
za uchaguzi Ibara ya 11 (2).
Kwa mujibu wa ibara hiyo, mrufani anapaswa kuwasilisha vielelezo vya rufaa yake, anuani ya kudumu na saini yake.
Lyato amesema, mrufani ameshindwa kutimiza matakwa hayo ya kanuni
pamoja na kushindwa kutokea kutetea hoja zake hiyo jana mbele ya Kamati
ya Rufaa.
“Kwa kuwa mrufani hakutimiza matakwa ya kanuni ya uchaguzi ibara ya 11
(2) ambayo inamtaka mrufani kuweka vielelezo vya rufaa yake, anuani ya
kudumu na saini yake.
“Kwa kuwa, mrufani hakutokea kutetea rufaa yake, kamati ya uchaguzi
imetupilia mbali rufaa ya Ishabakaki Luta,” ilisema taarifa hiyo.
Kutupwa kwa rufaa hiyo dhidi ya Manji, kunampa tiketi ya kushiriki uchaguzi huo wa
Julai 15, akichuana na wengine watatu
kwenye nafasi hiyo.
Mbali ya Manji, wengine wanaowania nafasi hiyo, ni Sarar Ramadhani, John Jembele na Edger Chibula.
Wagombea wa nafasi ya Makamu, ni Ayoub Nyenzi, Stanley Kevela ‘Yono,’ na Clement Sanga.
Wanaowania ujumbe ni Lameck Nyambaya, Ramadhan Mzimba, Mohamed Mbaraka, Ramadhan Saidi, Edger Fongo, Beda Simba,
Ahmed Gau, Mussa Katabalo na George Manyama.
Wengine ni Aaron Nyanda, Abdallah Bin Kleb, Omari Ndula, Shaaban
Katwila, Jumanne Mwammenywa, Abdallah Mbaraka, Peter Haule, Justine
Baruti na Abdallah Sharia.
Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi huo mdogo wa kuziba nafasi sita
zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali, kampeni zinaanza leo.
Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu
na nafasi nne za ujumbe wa Kamati ya Utendaji; baada ya watatu kujiuzulu na mmoja kufariki.
Mwenyekiti Lloyd Nchunga alijiuzulu Mei 23 mwaka huu kwa shinikizo la
Wazee na Vijana huku aliyekuwa Makamu wake, Davis Mosha
alijiuzulu Machi, 2011.Habari na Dina Ismail
No comments:
Post a Comment