BENKI ya CRDB imesema sasa wateja wa benki hiyo wanaweza kupata huduma za kibenki ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Ofisa Masoko, Ninaeli Munuo, alisema mbali na
hilo wanaweza kupata taarifa za kibenki kwa njia ya barua pepe.
Alisema katika tawi hilo lililopo ndani ya jengo, wateja wanaweza
kupata huduma ya ATM saa 24 katika kipindi chote cha Sabasaba.
Pia wateja wanaweza kufungua akaunti mbalimbali, huku ATM hiyo yenye
kutumia teknoloji ya kisasa inawawezesha wateja kuchukua pesa.
Aidha, inawapa fursa wale wasiokuwa na akaunti kufungua iwapo watakuwa na vitambulisho.
Alisema wapo wafanyakazi wa benki kwa ajaili ya kutoa msaada wa maelezo kuhusiana na huduma ya Simbanking.
Ofisa huyo aliongeza kwamba, benki imekuwa mstari wa mbele katika
kuwasogezea huduma za kibenki hivyo imeona ni jambo la busara la kutoa
huduma hizo ndani ya viwanja hivyo.
Aidha, aliongeza kuwa kwa sasa wameamua kutumia mbinu mpya ya kuwapatia taarifa za akanti kwa kupitia barua pepe.
Ninaeli aliongeza kwamba, mbal na yote pia wameamua kutumia mbinu
mpya ya kuwapatia taarifa za akanti kwa kupitia barua pepe. Kwa kuwa ni
njia ya haraka na urahisi ambayo inaepusha usumbufu.
“Zamani wateja walikuwa wanapata taarifa za akaunti zao kwa makaratasi, lakini kwa sasa wanaweza kupata
huduma hizo kwa njia ya barua pepe,” alisisitiza.
Hata hivyo baadhi ya wateja wa benki hiyo wameonekana kuridhishwa na utendaji wa benki hiyo kwenye viwanja vya Sabasaba.
Hata hivyo, benki hiyo imeonekana kung’ara katika maonesho kutokana na
wateja kupata huduma za kibenki ndani ya viwanja mara moja.
No comments:
Post a Comment