Precision
Air-Shirika la ndege linaloongoza Tanzania leo imerejesha safari zake
jijini Arusha kuanzia Julai 1 baada ya kusimamisha safari zake mapema
mwaka jana kwa ajili ya kupisha ukarabati wa uwanja wa ndege wa Arusha
iliyokuwa inaongezewa lami.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Bw.
Patrick Ndekana alisema kwamba shirika hilo la inafuraha kubwa kurejea
Arusha baada ya ukamilikaji wa ukarabati wa uwanja nambari 27 wa kurukia
uwanjani hapo ambayo itaruhusu ndege kubwa zaidi kutua na kuruka.
“Tunapenda
kuwataarifu wateja wetu kwamba tutaanza kuruka kwenda Arusha mara tatu
mpaka mara nne kwa wiki kuanzia Julai 1. Hizi safari zinatarajia
kukomesha usumbufu ambao wateja wetu wa Arusha wamekuwa wakipata kwa
kusafiri kwa gari kwenda na kurudi hadi uwanja wa kimataifa wa
Kilimanjaro kwa ajili ya kukamilisha safari zao,” alisema Ndekana.
Kurejea
katika soko hili itaimarisha utalii kwa sababu kutakuwa kuna usafiri
mrahisi wa kufikia jiji la Arusha ambayo inasifika sana kwa utalii.
Precision
Air pia imejidhatiti kutoa mtandao maradufu kwa wateja wake ili kuweza
kuwezesha shughuli za kijamii na kiuchumi kwa kuunganisha mikoa yote
nchini Tanzania.
“Arusha
ni moja ya miji mikubwa nchini Tanzania, ni nyumbani kwa mashirika
yakimataifa na sehemu yanoyotokea makongamano makubwa, bila kusahau
shughuli za kitalii. Mkoa huu kwahiyo unahitaji huduma ya usafiri wa
anga uliobora na ambao tunamiini sisi Precision Air tunaweza kuitoa,
kwahiyo tunapenda kuwa ahidi wateja wetu wategemee mambo makubwa kutoka
kwetu,” alisema Ndekana.
Uwanja
wa ndege wa Arusha imekuwa ikifanyiwa ukarabati kwa zaidi ya mwaka sasa
ili kuweza kufanya uwanja mzima kutumika baada ya kuongeza lami.
Marekebisho haya sasa yatawezesha ndege kubwa zaidi kutua na kuruka.
Wakati
huo huo, Bw. Ndekana pia ametangaza kwamba kuanzia Julai 1 2012,
shirika hilo litabadilisha muda wake wa kusafiri kwenda Johannesburg
kutoka saa 10 na nusu jioni hadi saa 4 kamili asubuhi ili kuweza
kuwapatia wasafiri urahisi wa kuunganisaha safari kwenda kwingine
wafikapo nchini Afrika Kusini.
Pamoja
na mabadiliko hayo, shirika hilo la ndege pia itaanza kutoa huduma ya
kuunganisha safari kutokea Johannesburg kwenda Kilimanjaro na Zanzibar
kupitia Dar es Salaam ili kuweza kuwapatia urahisi watalii. Hii
itafanyika mara 4 kwa wiki ambayo inamaanisha safari za Zanzibar na
Kilimanjaro zitaanza kuhudumiwa na ndege aina ya Boeing, wakati ATR
zikiendelea pia.
Ukiondoa
Arusha, Precision Air pia inasafiri kitaifa kwenda Mwanza, Bukoba,
Musoma, Kigoma, Kilimanjaro, Zanzibar, Mtwara na Dar es Salaam.
Kimataifa Precision Air inasafiri kwenda Lusaka, Lubumbashi,
Johannesburg, Hahaya, Nairobi, Entebbe na Mombasa. Via mrokim.
No comments:
Post a Comment