Watuhumiwa wawili wa mauaji ya mfanyabiashara na kusababisha vurugu
katika kata za Pasua na Bomambuzi Manispaa ya Moshi, jana wametoroka
wakiwa mikononi mwa polisi katika kituo kikuu cha polisi mjini Moshi.
Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo, zinaeleza kuwa kutokana na tukio hilo, polisi mmoja D/C Juma, anashikiliwa kituoni humo, kwa kosa la uzembe uliopelekea kumuachia mtuhumiwa huyo kutoroka akiwa chini ya ulinzi wake.
Watuhumiwa hao ni Archabodi Maleko (52) aliyekamatwa kwa kosa la mauaji ya muuza duka, Salutari Mallya (28) na kumjeruhi vibaya mmiliki wa duka hilo, Michael Mallya (52), huku mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina la Issa aliyeshikiliwa kwa kosa la kusababisha vurugu akitoroka wakati akihojiwa na polisi.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Julai 24, mwaka huu, ambapo duka la mfanyabiashara Hamfrey Male (36), liliibiwa fedha na mali, alifungua kesi polisi na kisha kwenda kuwatafuta Polisi Jamii wa mtaa wa Bomambuzi kwa jina maarufu ‘kunguru hafugiki’ na kuwapa kazi ya kumsaka mwizi wake.
Baada ya msako wa muda mrefu inadaiwa Male na Maleko, waliwaeleza kikundi hicho kuwa wanahisi wezi wao ni wanandugu hao, ambapo walikwenda hadi kwenye duka lao na kuanza kumshambulia Salutari na baadaye kumpigia simu Michael (kaka wa Salutari), ambaye alifika na kupatiwa kichapo kilichopelekea hali yake kuwa mbaya na hadi sasa yupo
hospitali Teule ya Mtakatifu Joseph eneo la Soweto mjini hapa.
Mtuhumiwa Maleko alitoroka baada ya polisi aliyepewa jukumu la kumpeleka katika hospitali ya Mtakatifu Joseph, kwa ajili
ya matibabu, aliporejea kituoni alimpa ruhusa ya kwenda nyumbani na kurejea asubuhi ya Julai 24, mwaka huu, aliporejea alifungua kesi dhidi ya watu waliompiga na kisha akatokomea.
Mtuhumiwa Issa alitoroka wakati akichukuliwa maelezo na askari polisi kwenye kituoni humo na hakuna askari anayeshikiliwa.
Aidha, baada ya tukio la mauaji na kujeruhi, tafrani kubwa iliibuka katika kata za Pasua na Bomambuzi, ambapo wananchi walianza kuwashambulia watu wanaodaiwa kufanya tukio hilo, ikiwemo kupita nyumba hadi nyumba wanamoishi vijana wa kikundi cha polisi jamii na nyumba za wafanyabiashara hao na kuharibu mali.
Hata hivyo, polisi walilazimika kutumia nguvu kwa kurusha risasi hewani na mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wanafanya vurugu na kuwakamata watu wanane kwa kusababisha vurugu na wafanyabiashara wawili kwa kosa la mauaji na kujeruhi.
Kundi kubwa la wananchi lilivamia nyumbani kwa Diwani wa kata ya Bomambuzi, ambaye ni Meya wa Manispaa hiyo, Jaffary Michael, ambaye aliwatuliza na kueleza msimamo wake ni kutaka sheria ichukue mkondo wake na hawalindi vijana hao.
Aidha, Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, akiongea na waandishi wa habari, alisema Jeshi hilo limetangaza donge nono kwa yoyote atakayewezesha kutiwa mbaroni kwa wahusika wa kikundi hicho, ambao mara baada ya tukio kutokea walikimbia kusikojulikana.
via NIPASHE

No comments:
Post a Comment