SERIKALI imesema ni kosa kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji kumkamata na kumuweka mtu mahabusu.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki, wakati akijibu swali la Mbunge wa Meatu, Meshack Opulukwa (CHADEMA), ambapo alisema Sheria ya Mahakama za Mahakimu Sura ya 11 inatamka na kutoa madaraka kwa baadhi ya watendaji kuwa walinzi wa amani, “Kwa mujibu wa sheria hiyo Maofisa Watendaji wa Vijiji hawakutajwa kuwa walinzi wa amani, kwa hiyo hatua yoyote ya Ofisa Mtendaji wa Kijiji kumkamata na kumuweka mtu mahabusu ni kosa kwa mujibu wa sheria za nchi na kuzuia uhuru wa mtu bila kuwa na mamlaka ni uvunjwaji wa haki za binadamu,” alisema Naibu Waziri.
Kuhusu Maofisa Watendaji wa Kata, alisema wao wamepewa pamoja na kazi zao nyingine za kila siku, jukumu la ulinzi wa amani ambalo kisheria linaambatana na madaraka ya kumkamata mtu aliyefanya kosa au kumuweka mahabusu kwa mujibu wa kifungu 53 cha Sheria ya Mahakama za Mahakimu sura ya 11 ili kusiwepo na uvunjifu wa amani.
Pia alisema kifungu cha 70 kinampatia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, mamlaka ya kuanzisha na kuzitembelea mahabusu zilizo katika maeneo yaliyokubalika na kuwa sheria inamruhusu Waziri kukasimu madaraka hayo kwa watendaji wa halmashauri walioteuliwa, “Kwa kuzingatia taratibu na sheria ya Mahakama za Mahakimu, natoa mwito kwa Watendaji wa Halmashauri hasa ngazi za vijiji kuwa makini na wanapotekeleza majukumu yao ili kulinda hali ya utulivu na amani katika maeneo yao,” alisema.
Pia alisema si ruhusa mtu kuwekwa katika maghala ya chakula au pamba kwani taratibu haziruhusu.
Katika swali la msingi Mbunge huyo alihoji hatua za baadhi ya watendaji wilayani Meatu kuwakamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali na kuwafungia mahabusu kwenye maghala ya chakula au pamba bila kuwapeleka mahakamani na kama hatua hiyo si kupingana na haki za binadamu.
via HabariLeo

No comments:
Post a Comment