EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, August 28, 2012

CHADEMA waendelea kujichanganya Uingereza - Clement Mbawala

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo jana kiliendelea kulalamikiwa na Watanzania kwa kukosa DIRA ya uongozi hasa baada ya kujichanganya,kubishana wenyewe kuhusu msimamo wa SERA yao hapa UK. Haya yaliwakuta katika kikao cha kutafuta wanachama kilichofanyika jana tarehe 27/08/2012 katika Mji wa Reading, UK.

Watanzania wachache waliohudhuria mkutano huo walinung'unika kuwa kikao hakikuwa na utaratibu na mtirirko wowote wa uendeshaji wa vikao na ulibagua uchangiaji wa kijinsia na ulijali zaidi ukabila.

Akilalamika huku akitoka nje ya ukumbi ndugu aliyejitambulisha kuitwa Said alisema kuwa Kikao hiki kiliandaliwa kwanza na Wachaga tu waliochangishana fedha na hivyo wakati wa kikao hawakutoa nafasi huru kwa watanzania wengi kushiriki kikamilifu zaidi ya kuambiwa watoe fedha kuchangia Chama na mfuko wa kuzikana.

Mwingine ni Bi Rehema aliyesema kuwa ameshangazwa na kauli ya Bw. Prudence aliyesema kuwa yeye ndiye ameachiwa jukumu la kueneza Sera na Siasa za CHADEMA na hivyo ni lazima achangishiwe fedha za kuzunguka UK ili aandae akina mama wasomi wajiunge Chadema ili wapewe nafasi za Ubunge wa Viti Maalum katika uchaguzi mpya 2015 maana wengi wa waliopo muda wao umekwisha na kuwa Viongozi wa Chadema wanajali kundi la akina mama. Nanukuu..''eti anatuambia mambo ya viongozi kujali wanawake na siyo Sera ya Chadema juu ya wanawake...yeye mwenyewe ametelekeza mke na watoto wake bongo..wanaomba omba tu huko yeye anakula raha na bado anataka michango yetu zaidi....jana tu alikuwa ndiyo kada mwandamizi wa CCM hapa UK akatengwa kwa sababu ya tabia zake...sisi siyo wajinga bwana..''

Ramadhani aliongea kwa mfadhaiko akishangaa kuwa Dkta Jona LUSINGU ni Wakala wa Chadema huku alikuwa ni Kiongozi wa Jumuiya ya Tanzania UK aliyeshindwa kazi na kukimbia uongozi mwenyewe bila kukabidhi ofisi na sasa atawezaje kusimamia siasa za Chadema ..''au ndiyo kuyeyushana tu..''. Alihamaki akiwa anatoka mlangoni na kuunyosha mkono kuelekea kwa Dk Lusingu aliyekuwa amekataliwa nafasi ya kukaa meza ya viongozi na hivyo kukaa na washabaki wachache waliokuwepo.

Alipopewa nafasi ya kuongea Dkt Lusingu alizidi kuwachanganya viongozi na mashabiki wachache waliohudhuria pale aliposema ''Chadema imekuwa haina sera ya Diaspora na Mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na Chadema kuingia madarakani Tanzania na hasa uongozi wao wa kitaifa uliopo sasa isipokuwa pale ambapo mfumo mzima wa utawala utakapobadilika na chadema kuwa chama cha kitaifa kuliko hivi sasa''. Aliongeza kwamba matawi ya nje ya Chadema yanaweza yasiwe na manufaa iwapo kama yatatelekezwa kama walivyofanya CCM.Aliongeza kuwa ni kweli toka Chadema imekuja hapa UK kumekuwepo na manung'uniko miongoni mwa Watanzania na ni vema kujipanga upya na uongozi msafi. Dkta Lusingu aliyekatishwa kuongea alikuwa ni mmoja wa viongozi wa awali wa shina la CCM Reading

MwanaCCM mmoja anayeitwa Chris alidokeza kuwa waliohudhuria mkutano huu sehemu kubwa ni wanaCCM walioingia kusikiliza kipya gani watani wamefuatia nazo nyayo lakini wameona hakuna jipya bali maumivu ya kukosa SERA. Alisema kuwa CCM UK imekuwa na mapendekezo mengi katika vikao vya Taifa na serikali imeanza kushughuliia kero nyingi za wanaDiaspora ikijumuisha kumalizia mpango mahsusi wa kueneza na kuleta UK huduma za kifedha na hifadhi za jamii kuliko danganya toto ya Chadema ya kuchangia mfuko wa mazishi..''yaani chadema wanaona umuhimu wa Mtanzania pale anapokufa tu na wao kumzika..'' Alidokeza kuwa ni uonevu kumtwisha mdogo wake Dkta Lusingu mzigo wa Chadema wa kuchangia vifo.. ''Wakati Jeladi Lusingu alipofiwa na mkewe ni wanaCCM waliongoza kuhimiza kufa na kupona miji yote ya UK ili kusaidia safari na hifadhi ya mwisho ya mama huyo. Leo sera za umoja zilizomsaidia anazipinga au amelazimishwa tu?''

Baada ya kikao kuisha Bw. Prudence alitamba kwa wenzake kuwa alipokuwa CCM UK kila mkutano walikuwa wakichangishana ili kuhudumia kikao na usafiri na sasa wanachama wamechoka kifedha na hivyo sasa Chadema imeanza kumwaga pesa kuwamaliza CCM kabisa hapa UK. Prudence alipoombwa mahojiano ya ana kwa ana alisema hana muda.

Mwandishi alitafuta na kupatiwa namba ya simu ya Mwenyekiti wa CCM UK ili kupata mawazo yake juu ya mkutano huu wa Chadema hapa Reading lakini alisema yupo Edmonton, London kuhudhuria CCM UK BBQ-Outreach Party iliyoandaliwa na wanaCCM North London tangu miezi miwili iliyopita hivyo asingeweza kuahirisha lakini anayo nafasi ya mahojiano baada ya siku hiyo. Pia alisema CCM ilikaribisha upinzani Tanzania na inaendelea kuikaribisha Chadema hapa UK.

Na Mwandishi wa kujitegemea,

Clement Mbawala.

Tanzania Now.

Slough.Berkshire.

''Empowering Diaspora by News''

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate