Rita Paulsen ‘Madam Rita’.
CHIEF Judge wa
Shindano la Epiq Bongo Star Search, Rita Paulsen ‘Madam Rita’ hivi
karibuni amejikuta akiombwa uchumba na vivulana nyenye umri mdogo
‘serengeti boys’ kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Akipiga stori na Ijumaa, Madam Rita alisema kuwa, alianzisha ukurasa huo kwa ajili ya kubadilishana mawazo na watu mbalimbali lakini akashangazwa na baadhi ya wavulana ambao wamempenda kiasi cha kufikia hatua ya kumuomba uchumba.

“Huwezi
amini sina siku nyingi sana tangu nimeanzisha ukurasa huu lakini nina
marafiki wengi na wapo ambao wanaomba kuwa marafiki wangu, huko
nimeshapata wachumba sita tena wengine wakiwa na umri mdogo sana,”
alisema Madam Rita na kuongeza:
“Kimsingi nawaheshimu watu wa rika zote kutoka mikoa yote kwani wao ndiyo wadau wakubwa wa EBSS na wameifanya program hii kujipatia umaarufu mkubwa na kufika hapa ilipo sasa.”

No comments:
Post a Comment