Bingwa
wa michuano ya BancABC Super 8 inayoanza keshokutwa (Agosti 5 mwaka
huu) katika miji ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha atapata
sh. milioni 40 wakati makamu bingwa sh. milioni 20. Pia timu mbili
zitakazoishia hatua ya nusu fainali kila moja itapata sh. milioni 15
wakati zilizobaki kila moja itapata sh. milioni 5.
Timu zimepangwa katika makundi mawili ya A na B. Kundi A lina timu za
Simba (mabingwa wa Tanzania Bara), Jamhuri, Zimamoto na Mtende zote za
Zanzibar. Kundi ni Super Falcon (mabingwa wa Zanzibar), Azam, Mtibwa
Sugar na Polisi Morogoro zote za Tanzania Bara.
Mechi za
ufunguzi keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) ni Simba vs Jamhuri (Dar es
Salaam), Zimamoto vs Mtende (Mwanza), Mtibwa Sugar vs Polisi Morogoro
(Arusha) na Super Falcon vs Azam (Zanzibar). Awali mashindano yalikuwa
yaanze Agosti 4 mwaka huu lakini yamesogezwa mbele kwa siku moja.
Hatua ya makundi itamalizika Agosti 12 mwaka huu. Mechi za nusu fainali
na fainali zote zitachezwa Dar es Salaam. Nimeambatanisha ratiba.
Mdhamini bancABC atagharamia usafiri wa ndege kwa timu zote kutoka
kituo kimoja hadi kingine, malazi na jezi. Yanga imejitokea kwenye
mashindano hayo na nafasi yake imechukuliwa na Mtibwa Sugar ambayo
ilishika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.
Taarifa kutoka TFF
Mechi za ufunguzi keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) ni Simba vs Jamhuri (Dar es Salaam), Zimamoto vs Mtende (Mwanza), Mtibwa Sugar vs Polisi Morogoro (Arusha) na Super Falcon vs Azam (Zanzibar). Awali mashindano yalikuwa yaanze Agosti 4 mwaka huu lakini yamesogezwa mbele kwa siku moja.
Hatua ya makundi itamalizika Agosti 12 mwaka huu. Mechi za nusu fainali na fainali zote zitachezwa Dar es Salaam. Nimeambatanisha ratiba.
Mdhamini bancABC atagharamia usafiri wa ndege kwa timu zote kutoka kituo kimoja hadi kingine, malazi na jezi. Yanga imejitokea kwenye mashindano hayo na nafasi yake imechukuliwa na Mtibwa Sugar ambayo ilishika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.
Taarifa kutoka TFF
No comments:
Post a Comment