Timu ya vijana ya Tanzania 'Ngorongoro Heroes' jana imekubali kichapo cha goli 2-0 toka kwa Nigeria, na kuondolewa katika kinyanganyiro cha kuwania kushiriki Mataifa ya Afrika kwa soka la vijana wenye umri huo kwa jumla ya goli 4-1.
Ngorongoro Heroes walikubali kufungwa na Nigeria goli 2-1 katika mchezo wa awali uliopigwa katika uwanja wa Taifa kabla ya leo kupokea kichapo hicho cha goli 2-0.
Matokeo hayo ya leo ni muendelezo mmbaya wa kocha mpya wa vijana Jakob Michelsen, ambapo ameiongoza timu hiyo katika mchezo wake wa nne na kupoteza michezo yote, ikiwa ni michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Rwanda na miwili ya mashindano dhidi ya Nigeria.
No comments:
Post a Comment