EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, August 13, 2012

Sakata la mtoto aliyeng`atwa na nyani `latinga` polisi

Baada ya sintofahamu kuhusu uamuzi wa kituo cha polisi Yombo Vituka, kutochukua malezo ya tukio la kung’atwa na nyani mtoto Abdul Idd (9), uongozi wa juu wa jeshi hilo umechukua hatua za kulishughulikia.
Abdul aling’atwa na nyani anayedaiwa kuwa moja ya wanyama pori wanaofugwa na mfanyabiashara mmoja, mkazi wa eneo la Yombo Lumo jijini Dar es Salaam.

Nyani huyo anadaiwa kutoka nje ya nyumba ya mfanyabiashara huyo ambaye jina lake halijafahamika, na kuwavamia watoto walipokuwa wanacheza mpira, miongoni mwao alikuwa Abdul, aliyevamiwa, kushambuliwa na kung’atwa mkononi.
Hata hivyo, tukio hilo lililoibuliwa na gazeti hili Jumapili iliyopita, liliwasilishwa kituo cha polisi Yombo Vituka, lakini askari waliokuwepo siku hiyo, hawakuchukua maelezo kwa ajili ya kufungua jalada ili mchakato wa kisheria wenye lengo la kudai haki itendeke.

Badala yake, askari hao walitoa taarifa maalum kupitia fomu namba tatu maarufu kama PF 3 ili mtoto huyo akapate matibabu.
Wazazi wa mtoto huyo, Idd Rashid na Aisha Suleiman, waliiambia NIPASHE Jumapili kuwa baada ya kuwasilisha taarifa hizo kwa gazeti hili, walirejea kituoni hapo na kuulizia mchakato wa kufungua jalada.
Walisema baada ya kudai haki ya kuchukuliwa maelezo, walijibiwa yalichukuliwa wakati wakihojiwa na kwamba yaliandikwa kwenye karatasi.
Kisha walipewa kumbukumbu yenye namba RB/1718/2012 ikiwa na kichwa kinachosomeka, “kushindwa kudhibiti mifugo.”

Hata hivyo, wazazi hao wanasema wanapofuatilia suala hilo polisi, wamekuwa wakijibiwa kuwa mhusika anayepaswa kuhojiwa, yupo safarini mkoani Morogoro.
“Tukienda wanatuambia kwamba mfanyabiashara anayefuga wanyama pori ambao polisi wameandika kuwa ni mifugo, yupo Morogoro, sasa hatujui cha kufanya,” alisema Idd katika mahojiano na NIPASHE Jumapili juzi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, David Misime, alipowasiliana na NIPASHE Jumapili mwishoni mwa wiki, alisema ofisi yake inashughulikia mambo mengi, hivyo apewe muda wa kuwasiliana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Temeke.
“Unafikiri mimi nina kila kitu hapa mezani kwangu, nipe muda nifuatilie kwa kuwasiliana na OCD (Mkuu wa Polisi wa Wilaya), niongee naye halafu tutawasiliana,” alisema.
Hata hivyo, hadi tunakwenda mitamboni, Misime hakupatikana kuelezea suala hilo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate