
 Baadhi
 ya wananchi wakiwa  wanaangalia mwili wa marehemu ambaye amepoteza 
maisha papo hapo mara  baada ya kugongwa na lori na kukanyagwa kichwa na
 hatimaye kupelekea  kichwa kupasuka na ubongo kumwagika chini leo 
majira ya saa tisa mchana  eneo la ilala boma

 
 
 Mwili
 wa marehemu  ambaye jina lake  halikuweza kufahamika mara moja ukiwa 
umefunikwa na kanga huku pembeni  vipande vya ubongo wake vikiwa pembeni
 mara baada ya kugongwa na lori na  kukanyangwa kichwa na kupelekea 
kichwa kupasuka na ubongo wote  kumwagika chini leo majira ya saa tisa 
mchana eneo la Ilala Boma. Kijana  huyu anasadikiwa kuwa ni mwanafunzi 
wa Darasa la Saba katika shule ya  Msingi Msimbazi.

 Askari
 wa Usalama barabarani  akisaidiana na baadhi ya wananchi kuubeba mwili 
wa marehemu ambaye jina  lake halikuweza kufahamika mara moja ili 
kuupakia katika gari dogo  tayari kuupeleka hospitali ya Amana.Kijana 
huyu anakadiriwa kuwa ni  mwanafunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya 
Msingi Msimbazi.

 Baadhi
 ya wananchi wakiutazama mwili  wa marehemu ambaye amegongwa na gari na 
kupelekea kupasuka kichwa na  kupoteza maisha papo hapo.

Mwili
 wa marehemu ukifunikwa vizuri  kwaajili ya kupelekwa hospitali ya 
amana.Pembeni ya mwili wa marehemu ni  vipande vya ubongo mara baada ya 
kukanyangwa na lori
Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog 
Kijana
 wa kiume ambaye jina lake  halikuweza kupatikana mara moja amepoteza 
maisha mara baada ya kugongwa  na lori leo majira ya Saa tisa Mchana 
eneo la Ilala Boma karibia na  Ofisi ya Mkuu Wa Mkoa wa Dar Es salaam. 
Mara baada ya kugongwa na lori,  lori hilo liliweza kukimbia na 
halikujulikana ni wapi limeelekea na  namba za gari hizo hazikuweza 
kupatikana mara moja.
Kijana
 huyu anakadiriwa kuwa na umri  wa miaka 14 ambaye pia shuhuda wa ajali 
hii ameueleza mtandao wa lukaza  blog kuwa ni mwanafunzi wa shule ya 
msingi Msimbazi Center kutokana na  sare za shule alizokuwa amevaa.
Shuhuda
 wa Ajali hii ambaye hakupenda  jina lake kuchorwa na mtandao wa LUKAZA 
amesema kuwa Wakati kijana huyo  anavuka barabara lori lililomgonga 
lilikuwa linatokea maeneo ya  buguruni na kumgonga kijana huyo. Mara 
baada ya kumgonga lilimkanyaga  kichwani " Lilianza tairi la mbele 
kumkanyaga kichwa halafu likafuatia  na tairi la nyuma ambapo 
lilipelekea kichwa kupasuka vibaya na hatimaye  ubongo kusambaa 
barabarani kama ambavyo unao hapo chini na hatimaye lori  hilo kukimbia"
 alisema shuhuda huyo.
LUKAZA BLOG ilimuuliza shuhuda huyo kwanini akunakili namba za usajili wa lori hilo
na
 hivi ndivyo shuhuda wetu  alivyojibu " Kiukweli Nilishindwa kuandika au
 kunakili namba ya usajili  wa lori kwasababu kwanza niliposikia kitu 
kizito kimegongwa na hilo lori  nilijua ni mtu wa bodaboda wakati 
naangalia vizuri nikaona ni kijana  mdogo ndiye amegongwa na lori 
likimkanyaga kichwa likiwa katika harakati  ya kukimbia hapo nilishindwa
 kuandika chochote kwasababu nilipigwa na  butwaa na kubaki kama 
bumbuwazi na mwili kushikwa na ganzi mara baada ya  kuona ubongo vipande
 vya ubongo chini" alisema shuhuda wetu
Mpaka
 mtandao wa lukaza blog  unaondoka eneo la tukio lori lililomgonga 
halikuweza kupatikana wala  kujulikana lilipoelekea na jina la kijana 
aliyepoteza uhai papo hapo  nalo halikuweza kupatikana  
Lukaza blog Inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliompoteza ndugu yao
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZO JUU 
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEPA PEPONI AMINA
Via Habari Mpasuko
sangafesto.blogspot.com 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment