TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DC Korogwe awajibishwe kwa udhalilishaji
Mtandao
wa Jinsia Tanzania (TGNP), tumesikitishwa sana na kauli iliyotolewa na
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Ndugu Mrisho Gambo, kwa mwanasheria
wa Halmashauri hiyo Bi. Najum Tekka, kuhusu uhalali wa shahada
aliyonayo hususan kuihusisha shahada hiyo na vitendo vya ngono! Kama
ilivyoripotiwa na vyombo vya habari ikiwepo gazeti la Majira Augosti 29,2012 Uk.3
Kauli
hii ni udhalilishaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za wanawake na
inaenda kinyume na misingi ya kuzingatia usawa sanjari na Katiba ya
nchi ; Uwezeshaji wa wanawake na utekelezaji wa Maazimio ya Haki na Usawa katika ngazi za Kimataifa Kikanda na Nchini Tanzania.
Aidha kauli hii, inalenga kupotosha na kukatisha tamaa juhudi kubwa wanazofanya wanawake na wasichana katika kupata
elimu na mafanikio mbalimbali nchini Tanzania. Zaidi ya hapo, kauli
hii inadhalilisha na kushusha hadhi ya vyuo vya elimu ya juu
vinavyofanya kazi kubwa ya kutoa elimu kwa Watanzania.
Kutokana na kauli hiyo DC amekiuka
maadili ya uongozi wa umma na kukidhalilisha kiti cha ukuu wa wilaya
na kiongozi Mkuu wa nchi aliyemteua kushika wadhifa huo. Aidha kauli ya
kiongozi huyo ya kutimia mahakama kutetea hoja yake , kunaashiria ubabe , ujeuri, vitisho, kiburi na dharau ya kutaka kuingilia uhuru wa mahakama na ajenda binafsi isiyokuwa na maslahi kwa wanawake na umma wa Watanzania
Kutokana na kauli hiyo ya udhalilishwaji ,sisi wanaharakati wa ukombozi wa wanawake Kimapinduzi, usawa wa kijinsia, haki za kibinadamu demokrasia tunalaani vikali kauli za DC na kutoa Rai ifuatayo:
1. Mkuu wa Wilaya Ndugu Mrisho: amwombe radhi Mwanasheria Bi. Najum Tekka, kwa kosa la kumdhalilisha kijinsia
2. Tume
ya maadili ya utumishi wa umma, na Mamlaka nyingine za kinidhamu
zimchukulie hatua za kinidhamu Ndugu Gambo kwa kutumia lugha ya
kudhalilisha watumishi kinyume na maadili.
3. Wanawake wote, wanaume, vijana wa kike na kiume kuendelea na mapambano dhidi ya mfumo dume na mifumo yote kandamizi, kushikamana katika kudai misingi ya kisheria, uwajibikaji inayozingatia usawa na haki na kukataa kudhalilishwa katika ngazi binasfi na za umma !.
Imetolewa Dar es salaam leo 31/08/2012 na:
Usu Mallya
Mkrugenzi Mtendaji TGNP
No comments:
Post a Comment