MKAZI wa Kijiji cha Kasisa Kata ya Nyakasungu wilayani Sengerema, Shija Daudi (32) amejiua kwa kujinyonga na kamba hadi kufa usiku wa kuamkia jana baada ya kupima afya yake na kugundulika kuwa na Virusi Vya UKIMWI (VVU).Akizungumza na HabariLeo Jumapili jana akiwa nyumbani kwake mjini hapa, Isack Daudi alisema kuwa Daudi alikuwa amekwenda nyumbani kwake kuwasalimia lakini akiwa bado yuko nyumbani kwake alishikwa na maradhi ya kuumwa homa ya mara kwa mara iliyoambatana na malaria kwa muda wa wiki mbili.
Alisema baada ya kuona hali hiyo aliamua kumpeleka katika Zahanati ya Nyerere iliyoko Buswelu, lakini hali iliendelea kuwa mbaya na ndipo alipoamua kwenda kupima afya yake katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure ndipo alipogundulika kuwa na VVU, “Baada ya kubaini hayo, alijiunga na huduma ya tiba kwa kupewa ushauri nasaha na akawa anatumia dawa za kurefusha maisha za ARV kama kawaida,” alisema Isack.Alisema juzi akiwa anatoka kwenye mazishi ya jirani yake katika Mtaa wa Buswelu ghafla alikutana na watoto wake ambao walikuwa wanakimbia huku wakimueleza kuwa ndugu yake Shija alikuwa amejifungia ndani ya chumba,
“Nilichukua pikipiki nikakimbia kwenda nyumbani nilipofika nilikuta yumo ndani amejifungia ndani na nilibisha hodi mara tatu bila kuniitikia ndipo nilipoamua kubomoa dirisha na nilipoingia ndani nilimkuta amening’inia, alikuwa amejiua na siku ile baada ya kumpima alisema haoni raha ya kuishi tena duniani, inaonekana alichukua maamuzi ya kujinyonga,” alisema Isack kwa masikitiko.
Anasema baada ya tukio hilo, aliamua kumpigia simu Balozi wa Mtaa wa Buswelu A, Turubuza Millinde na baada ya kufika alishauri apigiwe Mwenyekiti wa Mtaa, Meshack Budega ambaye alichukua jukumu la kumpigia simu Mkuu wa Kituo cha Polisi cha MwaTex kilichoko Nyakato, “Alikuja OCS na askari wenzake ambao walishuhudia tukio hilo na baadaye OCS alitushauri mwili upelekwe kituoni, kwake kwa ajili ya maelezo zaidi ikiwemo kufanyiwa uchunguzi zaidi na tunawashukuru polisi kwa ushirikiano waliotupatia kama familia na baada ya pale mwili ulipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya Bugando,” alisema.
via HabariLeo
No comments:
Post a Comment