EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, September 16, 2012

Jukwaa la Waandishi wa Habari Waislam kuzinduliwa Dar es Salaam wiki ijayo

JUKWAA la Waandishi wa Habari wa Kiislamu Tanzania (NAMJOF) litazinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam, wiki ijayo, Mratibu wa Jukwaa hilo, Hemed Adam Kimwanga alisema jana.

Kimwanga aliongeza kuwa, mahali na siku rasmi ya uzinduzi huo vitatangazwa wakati wowote na amewaomba waandishi wa habari wa Kiislamu kuwa tayari kujumuika kwa ajili ya kulizindua jukwaa hilo.

“Kwa hakika kwa sasa lazima jukwaa hili lianze rasmi kufanya kazi zake”, alisema Kimwanga ambaye ameasisi nia hiyo tangu mwaka 2007 mara baada ya kumaliza mkataba wake wa kikazi kwenye Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) akiwa Meneja Uhusiano na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Baraza hilo.

Amesisitiza kuwa matukio ya hivi sasa ya vurugu za Kiislamu nchini yamesababisha kuwepo umuhimu mkubwa na wa haraka wa kuwepo NAMJOF ili kuipeusha jamii ya Kiislamu na jamii nyingine na migongano isiyokuwa ya lazima.

Amesema kwamba madhumuni makubwa ya jukwaa hilo ni kuwawezesha waandishi wa habari wa Kiislamu kuijua vyema dini yao na fikra zake sahihi ili kuandika kwa usahihi mambo yote yanayoihusu dini ya Kiislamu kinyume cha ilivyo sasa ambapo inaonekana kuna mvurugano mkubwa wwnyw malengo ya kimaslahi ya kibinadaamu zaidi kuliko ya dini yenyewe.

“Tusipoliangalia hili litatugharimu wote huko mbele ya safari”, amesema Kimwanga na kusisitiza kuwa ni NAMJOF imara ndiyo itakayosaidia kuepusha uvunjifu wa amani ya nchi unaonekana dhahiri kulijongelea Taifa hivi sasa, “Huwezi kumng’oa Mifti iwapo wewe humo ndani ya ulingo wa uongozi rasmi wa BAKWATA”, alisema Kimwanga na kuongeza, “Mufti anaondolewa na vikao rasmi ndani ya Baraza hilo”.

Amesema chini ya katiba ya BAKWATA, Mufti anang’olewa baada ya kikao cha masheikh waTanzania nzima kijulikanacho kama ‘Tume ya Dini’ wanaotambulika na Baraza hilo kumjadili na kupeleka mapendekezo yao kwenye Mkutano Mkuu ambao utaidhinisha au kupinga mapebndekezo ya Tume ya Dini kwa zaidi ya robo tatu ya kura zote za wajumbe halali, “Kinyume cha hapo utakuwa ni uhaini mkubwa ambao hauwezi kuvumiliwa na wapenda amani wakiwemo Waislamu na wasiokuwa waislamu”, alisisitiza.

Alisema waandishi watakapoelewa dini yao, katiba ya BAKWATA na katiba mama ya nchi, hapana shaka utulivu utatopea nchini na hivyo kuongeza ustawi wa kizazi kilichopo na kijacho cha Kiislamu na ksichokuwa cha Kiislamu hapa nchini na nje ya nchi, “Kwa kitendo cha kuwavuruga na kuwapotosha waumini wa dini ya Kiislamu kuhusu sensa na hiki cha sasa cha kutaka kumng’oa Mufti kutoka madarakani ni ushahidi mkubwa kuwa waumini wa dini ya Kiislamu wanatakiwa wapewe elimu sahihi ya dini yao na kanzu zake zinazoizunguka na hilo ndilo jukumu la NAMJOF”, alisIsitiza Kimwanga.
RasImu ya NAMJOF tayari imetayarishwa na Kimwanga alisema moja ya mambo makuu yatakAyojadiliwa ni kuipitia rasmi hiyo ili ikipita isajiliwe kwa kulihuisha rasmi  jukwaa hilo kisheria za za nchi.
Alisema tayari kuna taasisi zimeonesha utayari wa kutoa semina za kidii, kiutawala na uongozi kwa waandishi wa habari wa Kiislamu chini ya NAMJOF ili jukwa hilo lifanye kazi zake kwa usahihi na maendeleo chanya ya dini ya Kiislamu na jumuia nyingine hapa nchini na nje ya nchi.

Bila kuzitaja taasisi hizo, Kimwanga alisema NAMJOF pia itakuwa na Idara mbalimbali na kamati rasmi za masheikh, kinamama, vijana na nyingine na kwamba kutakuwa na idara za kidini na kidunia kwa faida ya waandishi wa habari wa Kiislamu na Taifa zima, “Tutakuwa na kamati ya Masheikh sita ambao watakuwa mhimili mkubwa wa jukwaa letu katika kutafsiri mienendo ya dini ya Kiislamu na saikolojia yake”, alisema Kimwanga.

Alipoulizwa kuhusu kadhia ya Mufti kung’olewa madarakani, Kiwamnga alisema, kwa niaba ya NAMJOF, anapinga vikali azma hiyo na kusema kuwa wanaotaka kufanya hivyo wanamkosea Mwenyezi Mungu aliyeamrisha waumini wa dini ya Kiislamu kumuheshimu na kumtii yeye kwanza, Mtume wake Muhammad (SAW) na wale wote walioko juu ya mamlaka ikiwemo serikali na viongozi wa dini.

Alisema kikatiba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA), Mheshimiwa Mufti bado hajavunja kipengele chochote ambacho kingehalalisha kuondolewa kwake. Chini ya katiba ya BAKWATA, Mufti anaondolewa iwapo atapoteza sifa kama vile kurukwa akili, kuwa mlevi, kuwa mzinzim, kuwa muongo na iwapo atabadili dini, “Hivyo hao wanaotaka kumng’oa Mufti madarakani wanafanya uhaini mkubwa wa mchana peuepe pee”, amesisistiza Kimwanga na kuishukuru serikali na vyombo vyote vya ulinzi na usalama kwa kumlinda Mufti na viongozi wengine wote wa BAKWATA wasipokwe madaraka yao waliyoyapata kikatiba.

Falsafa ya kuwa na chombo cha Waandishi wa Habari wa Kiislamu nchini iliasisiwa na mwandishi mkongwe nchini, Swalehe Msuya wa Daily News na baadaye Radio Tanzxania kwenye miaka ya themanini.

Baadaye mapema kwenye miaka ya 2000, mwandishi mwingine mkongwe na fundi mitambo wa Radio Tanzania Dar es Salaam, Athumani Mahanyu alijaribu kuanzisha chama cha aina hiyo lakini akaishia kuwa muasisi wa Radio Sauti ya Koran inayomilikiwa na BAKWATA kwa sasa,
Waandishi wote hao wawili Msuya na Mahanyu kwa sasa ni marehemu.

HabariMseto blog

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate