EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, September 30, 2012

Mke wa askari jela miaka 12 kwa kumteka binti aliyeishia danguroni.

SAKATA la binti aliyetoroshwa kutoka mjini hapa akiwa darasa la saba na kupelekwa kwenye danguro mjini Mbeya, limeisha kwa mke wa askari Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha mjini hapa, Christina Kanoni kutupwa jela miaka 12, akihusishwa na tukio la `kutekwa’ kwa binti huyo.

Hata hivyo, pamoja na hukumu hiyo, binti huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 14, amehuzunika akisema angekuwa hakimu, angemhukumu Kanoni kifo akidai ni binamu yake na katili sawa na muuaji.

Binti huyo mkazi wa Majengo Tanesco mjini hapa, alitoroshwa mwaka jana kwa kulishwa chakula kinachodaiwa kuwekwa dawa za kulevya na alizinduka akiwa Mbeya ndani ya danguro lenye wasichana zaidi ya 30, wote wakitumikishwa kwa biashara ya ngono.

Akizungumza baada ya hukumu ya Septemba 18 iliyotolewa na Hakimu Rosalia Mugisa wa Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga, binti huyo alisema adhabu hiyo ni ndogo ikilinganishwa na alivyotendwa.

“Huyu hakuwa binadamu wa kawaida, ni binamu yangu lakini nadhani alistahili adhabu zaidi ya kifungo cha miaka 12,” alisema huku akisikitika kuachishwa shule lakini kibaya zaidi, kuingizwa katika biashara haramu ya kutumikishwa kingono kwa takribani miezi saba, kila siku akikutanishwa na wanaume zaidi ya wawili.

Siku ya hukumu, Hakimu Mugisa alisema ameridhishwa pasipo shaka na ushahidi wa upande wa mashitaka ulioongozwa na
Mwendesha Mashitaka Matiku Matiku kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo. Akisoma hukumu, alisema: “Licha ya kutoa utetezi kuwa wewe (mshitakiwa) ni mjamzito, lakini bado nakuhukumu kwenda jela miaka 12 au kulipa faini ya Sh milioni 12 … adhabu hii kali iwe fundisho si kwako tu bali pia kwa wengine wenye tabia kama yako. Kitendo ulichokifanya si tu cha kinyama, lakini pia ni cha kikatili na chenye machukizo makubwa mbele ya jamii.” Wakati binti huyo akionesha kutoridhishwa na adhabu hiyo, baba yake mzazi, Michael Ndasi, babu, Edwin Ndasi (66) ambaye ni Mganga Mfawidhi katika zahanati ya Pito mjini hapa na mkewe, Lilian Ndasi (54), muuguzi wa zahanati ya Majengo waliridhika na hukumu hiyo, wakisema itakuwa fundisho kwa wengine.

Awali mwendesha mashitaka, Mkaguzi wa Polisi, Matiku, alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 09, 2011 eneo la Majengo mjini hapa kwa kumrubuni msichana huyo na kumsafirisha na kumwuza Mbeya kutumikishwa kwa ngono.

Upande wa utetezi uliita mahakamani hapo mashahidi wanne akiwamo binti mwenyewe ambao walitoa ushahidi ulioiridhisha mahakama hiyo.

Binti huyo ambaye hakuhitimu elimu ya msingi baada ya kukatizwa masomo akiwa darasa la saba alikuwa tayari amesajiliwa kufanya mtihani akiwa na umri wa miaka 13, alisema tangu aingizwe katika ukahaba, hafikirii kurudia shule ya msingi, na badala yake anataka aanzie kidato cha kwanza akidai ana uwezo wa kumudu masomo.

Alisisitiza kuwa, kama akibahatika kusoma sekondari, atapenda kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanasheria ili asaidie wanyonge wanaoteseka kwa kukosa haki nchini.

Bibi wa binti huyo alikiri kuwa mjukuu wake alikuwa na uwezo mkubwa darasani na yuko tayari kumsomesha, lakini kwa masharti ya kupata shule ya bweni au hosteli yenye ulinzi mkali kwa alichosema mjukuu wake ameshaharibiwa kwani hashikiki kwa wanaume, kiasi cha wakati mwingine kutolala nyumbani.

“Nakiamini kichwa chake, lakini kisaikolojia hayuko sawa, anahitaji uangalizi wa karibu mno. Kwa sasa anapenda sana ngono, nashukuru afya yake ni njema, tumemfanyia vipimo kwa kweli hajapata maambukizi ya UKIMWI. Tunafikiria kumpeleka kwa wataalamu wa saikolojia,” alisema bibi huyo. 

Lakini binti akisimulia suluba alizopata katika danguro mjini Mbeya, alisema katika miezi yote saba, kuanzia siku aliyoondolewa usichana wake kwa lazima akiwa na umri wa miaka 13, hakufurahia maisha.

Alisema siku zote, yeye na wenzake walifungiwa kwa tajiri wakilindwa na walinzi watatu usiku na mchana, ingawa usiku walikuwa wakitolewa kwa kusambazwa kwenye baa na majumba ya starehe kuuza miili yao chini ya ulinzi mkali wa wapambe wa ‘tajiri’.“Nilikuwa nalala ‘chapchap’ na wastani wa wanaume wawili usiku mmoja…matajiri wangu walikuwa wakinipeleka kwenye nyumba ya kulala wageni kwa muda, huku kila mteja akitozwa Sh 10,000 ... niliishi maisha hayo ya kuchukiza na machafu ya ukahaba kwa miezi saba hadi nilipofanikiwa kutoroka na kurudi nyumbani,“ alisema na kuongeza kuwa, ujira ulikuwa chakula, nguo na viatu kwa ajili ya kutokea usiku.

Aliongeza kuwa ajira hiyo isiyo rasmi mjini Mbeya ilikuwa kama sehemu ya mafunzo, kwani walioonekana kukomaa katika ukahaba, walikuwa wakisafirishwa nje ya nchi, akitoa mfano kuwa siku chache kabla ya kutoroka, wenzake 10 waliaga kuwa safari ya Urusi kwa ajili ya kazi hiyo imewadia.Alisema alitoroka nyumba hiyo ya mateso baada ya kumwibia tajiri Sh 30,000 na kumrubuni mlinzi kisha kuondoka Julai 3 mwaka jana, bila kujua mwelekeo hadi aliposaidiwa kufika kituo cha mabasi mjini Mbeya alikopata usafiri wa kumrudisha hapa.
Habari via gazeti la HabariLeo

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate