Mmoja wa viongoi wa maandamano hayo jina lake halijaweza kupatikana kwa haraka akiwahimiza waislam wenzake kuto kukata tamaa moaka kieleweke. Hapa wakiwa mbele ya jengo la wizara ya Mambo ya ndani kama linavyoonekana kwa mbele
Wakina mama wa kiislam nao hawakuwa nyuma katika maandamano hayo wakishinikiza waislam wenzao waliokamatwa kwa sababu ya kugoma kuhesabiwa watolewe, mpaka hivi sasa tunaingia mitamboni bado waandamanaji hao wapo katika jengo hilo la Wizara ya mambo ya ndani.
Wanahabari nao hawakua nyuma katika kupata picha za tukio hilo
Kwa juu kwenye gorofa ni wafanyakazi wa Benk ya Exim iliyo karibu na Wizara hiyo wakiwa hawajui la kufanya huku wengi wao wakihofu kama mabomu ya machozi yakianza kupigwa watajisalimisha wapi, huku waislam kama unavyowaona kwa chini wakiwa wanaimba nyimbo mbali mbali za kuhamasishana kama iivyozoeleka kwa usemi wa kiimani yao "TAKHBIIRRR!!!!"
Hapa wakiwa wanaelekea kwenye wizara ya mambo ya Ndani.
Tikio hilo limetokea muda mfupi uliopita. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ambayo imetolewa na jeshi la polisi kutokana na maandamano hayo.
Rais wa Tamsia Taifa, Sheikh Jaffar Said Mneke (katikati), akiongea na waandamanaji mara baada ya kumaliza kikao na viongozi wa wizara.
Baadhi ya Waislamu jijini Dar es Salaam leo wameandamana kuelekea Wizara ya Mambo ya Ndani kutaka wenzao waliokamatwa wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linaloendelea nchini kuachiwa. Katika maandamano hayo viongozi wa Waislamu na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani walikutana na kufikia makubaliano kuwa wote waliokamatwa wakipinga zoezi la Sensa Zanzibar na Tanzania Bara wataachia huru. Pia waandamanaji hao wamekubaliana kufanya maandamano mengine ya kumng'oa Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaban Bin Simba kwa kutoonesha ushirikiano nao.
No comments:
Post a Comment