FULL TIME: Yanga African 1 - 1 Simba SC
Magoli (Bahanuzi DK 65 na Amri Kiemba DK 4)
DK94: Juma Kaseja anaokoa shuti kali la Saidi Bahanuzi
DK89: Kavumbagu wa Yanga amekosa goli la wazi.
DK88: Juma Nyoso wa Simba amepewa Kadi ya Njano
DK88: Simba wanafanya mabadiliko, ametoka Mwinyi Kazimoto ameingia Ramadhan Chombo Redondo.
DK87: Yanga 1 - Simba SC 1
DK82: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Kevin Yondan ameingia Juma Abdul
DK79: Simon Msuva wa Yanga apewa kadi nyekundu baada ya kumpiga teke Nyoso wa Simba.
DK70-DK72: Belko amepata maumivu, amelala chini kwa muda wa dakika mbili na mpira umesimama.
DK69:Simba wanafanya mabadiliko..anatoka Jonas Mkude anaingia Haruna Moshi Boban
DK65: Bahanuzi aipatia yanga bao la kusawazisha
DK 64:Yanga wapata penati
DK 60: Yanga wanalishambulia lango la Simba na Didier Kavumbagu anabaki na Kaseja na kupoteza nafasi ya kufunga goli la kusawazisha.
DK 55: Juma Kaseja anagongana na Kavumbagu aliyeingia kuchukua nafasi ya Nizar, napata maumivu yanayosababisha mpira kusimama.
DK 50: Simba 1 - 0 Yanga
DK 46: Niyonzima anapoteza mpira kwenye lango lao na unaenda kwa Kiemba anayepiga shuti kali na kama sio umahiri wa Yew Berko lingekuwa bao la pili.
Kipindi cha pili kinaanza hpa uwanja wa taifa.
DK 45: Mpira ni mapumziko Simba 1 - 0 Yanga
DK 40: Simba 1 - 0 Yanga
DK 35: Yanga wamebadilika sasa wanalishambulia sana lango la Simba, huku Simba wakipoteza mipira hovyo, hasa mshambuliaji Edward Christopher anazidiwa ujanja na Mbuyu Twite kila mara.
DK 31: Mbuyu Twite anapiga shuti kali linagonga mwamba na kurudi uwanjani.
DK 28: Edward Christopher anapewa kadi ya njano kwa kujiangusha kwenye eneo la penati.
DK 25: Yanga wanaonekana kubadilika ndani ya dakika hizi, wanatumia zaidi upande wa kushoto wa Simba kupitisha mashambulizi.
DK 20: Simba 1 -0 Yanga
DK 16: Yanga wanapata kona ya kwanza katika mchezo huu, ambayo inapigwa lakini Mwasyika anapiga shuti linapiga nyavu za nje.
DK 14: Simba wanaendelea kutawala safu ya kiungo hivyo kulishambulia mara kwa mara lango la Yanga. Mpaka sasa Simba wameshaingia kwenye lango la Yanga kwa zaidi ya mara 6 huku Yanga wakiwa hawajafanya shambulizi la kutisha kwenye lango la Kaseja.
DK 10: Timu zinashambuliana kwa zamu ingawa Simba wanaonekana kumiliki mpira zaidi. Simba 1-0 Yanga.
Dakika ya nne Amri Kiemba anaipatia Simba bao la kwanza kutokana krosi safi ya Saidi Chollo.
Mchezo ndio unaanza hapa uwanja wa taifa.
KIKOSI CHA SIMBA KINACHOANZA
Kaseja, Nassoro Masoud, Paul Ngalema, Shomari Kapombe, Juma Nyosso, Jonas Mkude, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Edward Christopher na Amri Kiemba. MFUMO 4-3-3
KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA
Yaw Berko, Mbuyu Twite, Stephano Mwasika, Nadir Haroub, KelvinYondani, Athumani idd , Nizar Khalfan, Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Said Bahanuzi
BENCHI: Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Godfrey Taita, Stafano Mwasyika, Job Ibrahim, Frank Domayo, Shamte Ally, Idrisa Rajab na Jerry Tegete.
SIMBA B 2 - 2 YANGA B
Katika kuelekea mtanange wenyewe hapo saa moja jioni, jioni hii timu za pili za Simba na Yanga zimetoka sare ya mabao mawili kwa mawili katika mchezo wa utangulizi. Yanga walianza kufunga mabao yote mawili katika kipindi cha kwanza kabla ya Simba kurudi vizuri kipindi cha pili na kurudisha magoli yote.
AMIR MAFTAH - TUNASHINDA
Simba imeingia uwanjani saa 11.15 kisha Yanga wakafuatia dakika chache baadae. Kiujumla hali ya uwanja ni nzuri na tayari shamra shamra za mashabiki kutambiana zinaendelea, wakati wale wa Yanga wakidai ni lazima washinde katika mchezo unaotaraji kuanza saa moja kamili jioni ya leo.
Mtandao huu umekutana na beki ambaye hatoweza kucheza katika mchezo huu, Amir Maftah ambaye amekiri kuumizwa na kuukosa mchezo huo, Maftah ambaye alikuwa na haraka ya kuingia uwanjani alisema tu kwa kifupi" Mechi hii tutashinda" alisema Maftah muda mfupi uliopita alipokutana na mtandao huu uwanjani hapo. Mashabiki wa Simba wameonekana watulivu kuliko wale wa Yanga
No comments:
Post a Comment